Thursday, December 5, 2013

PICHA ZINATISHA SANA: MZEE MMOJA AGONGWA NA GARI NA KUSAGIKA MGUU ALIPOKUWA ANAVUKA BARABARA,MZEE huyu wa jamii ya kabila la wamasai aliyetambulika kwa jina la ''Tulito'' Mkazi wa KIA njia panda ya kuelekea uwanja wa ndege wa Kilimanjaro International Airpot, amepata ajali mbaya ya kugongwa na fuso alipofanya jaribio la kuvuka barabara hiyo ya lami ambayo magari huenda mwendo kasi.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka mkoni kilimanjaro kimedai kwamba gari hilo aina ya FUSO halikusimama baada ya kumgonja mzee Tulito, lilitokomea..! Raia waliokuwa karibu na eneo la tukio hawakufanikiwa kunasa hata namba za gari hilo, Mzee tulito aliwahishwa Hospitali wilayani boma kwa matibabu zaidi.


CHANZO : MATUKIO NA MICHAPO