Wednesday, December 4, 2013

SHEREHE ZA UHURU WA TANGANYIKA NEW YORK CITY JUMAMOSI TAREHE 7

Watu wote mnakaribishwa siku hii ya uhuru kutakuwa na vyakula, vinywaji music na mambo mengi ya kuchangamsha. Unachotakiwa ni kulipa 30$ tu mlangoni njoo tusherekehe siku yetu watanzania kufika kwenu ndiyo mafanikio ya sherehe hii. Sherehe zitaanza saa 11 na nusu jioni njoo mapema uwahi meza yako, usije kula chakula na kunywa ukiwa umesimama chakula kikakimbilia miguuni na ukashindwa kucheza music. Ma DJ wetu bora watatuchezesha mwendo wa ndombolo na rusha roho hadi kukuche, vaa kiafrica kuonyesha uzalendo Wote mnakaribishwa. Ukitaka kufika kwa kutumia train chukua N, Q kwenda Queens  hadi 36Th Street, Na tembea mtaa mmoja hadi 37Th St kunja kulia jengo litakuwa mkono wako wa kushoto.
Ticket zimeanza kuunzwa mbele ya desk la Tanzania Mission New York. Na pia unaweza kupa ticket hizo kupitia kamati ya maandalizi ya sherehe hiyo ya uhuru, kwa kupiga # hizi za simu, #347 663 0781, #917 557 3195, Pata ticket yako sasa.
 Address
 Claudio's Cafe II,
 32-23 37th Avenue. 
Astoria, NY 11101
Siku hiyo ya Uhuru wa Tanganyika kutakuwa na Nyama choma kutoka kwenye jiko la kisasa la Temba Engineering Service. Jiko linalochoma nyama kwa kiwango cha hali ya juu kabisa, njoo na uonje nyama iliyochomwa na jiko hilo la kisasa linalotumia computer maalumu inayokujulisha kuwa nyama imewiva kwa kiwango kinachotakiwa kuliwa na binadamu bila kuleta madhala yeyote.

New York Tanzania Tema wako fit kwa mchezo.
Uwanja ni huu utakaomaliza ubishi  wa mchezo wa kirafiki kati ya New York na New England (Umoja) Springfield Boston hapa New York wachezaji kuwahi mapema mchezo utaanza saa 8 mchana.   Katika uwanja wa 

Aviator Sports And Event Center 
Address 
3159 Flatbush Avenue ,
 Brooklyn.Ny 11235. 
Team ya New York baada ya kujifua sana huu ni mchezo wao wa kwanza, wachezaji wamejipanga vizuri ili kuwafundisha mpira team ya Springfield. Baada ya majigambo ya pande mbili kila mmoja akisema ni zaidi ya mwenzie sasa siku ya uhuru jumamosi ya tarehe 7 mzizi wa fitina unakatwa, ukisikia PAHHHHHHHHH labda itokee tuuuuuu!!!

No comments:

Post a Comment