Sunday, December 8, 2013

SHEREHE ZA UHURU WA TANGANYIKA ZAFANA NEW YORK

 Meza kuu ya waheshimiwa ikiongozwa na Mheshimiwa

Tuvako N. Manongi Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katika kusherehekea siku hii ya uhuru wa Tanganyika Watanzania walikula, kunywa na kucheza hadi majogoo. Licha ya kula, kunywa na kucheza kulikuwa na mambo mengi kama fashion show ya nguo za kiafrika, nguo ambazo zimebuniwa na Bea Lunjwangana na kusimamiwa na Jessica Lujwangana na pia watanzania walipata fursa ya kusikia historia ya uhuru wa Tanganyika kutoka kwa Bi Ashura.
Mh.Balozi Manongi akiongea mbele ya Watanzania walikuwepo ukumbini hapo kusherehekea siku ya Uhuru wa Tanganyika. Sherehe zilifanyika New York na kuuzuliwa na Watanzania waishio Ny, Boston, Ct, Jr na Pa.
Bi Ashura akielezea jinsi anavyoikumbuka siku hii ya uhuru.
Katibu wa New York Tanzania Community bwana Mhella 
Mwenyekiti wa New York Tanzania Community Bwana Hajji Khamis akimkaribisha Mh. Balozi Manongi
Washereheshaji Gaston na Hadiatou wakielezea kila kinachojiri ukumbini hapo
Joyce na Mauris wakiongoza uimbaji wa wimbo wa taifa ukumbini hapo.
Mh. Balozi Manongi akikata keki ukumbini hapo. Kwa picha zaidi nenda soma zaidiDj Rich kutoa Springfield Ndiyo habari ya mjini akiwa busy nyuma ya mashine kuwapagawisha watu ukumbini hapo, Ukumbini palikuwa hapatoshi kwani Dj Rich aliwachezesha mwanzo mwisho.