Tuesday, March 25, 2014

JE UNAMFAHAMU MICHAEL AGUSTINE LUKINDO? TAFADHALI WASILIANA NASI

Habari jamani. Ninaandika ujumbe huu kwa kuomba msaada. Mtanzania mwenzetu amefariki in Madison Wisconsin-USA, wanatafutwa ndugu zake. Ni mtu wa Tanga,MICHAEL AGUSTINE LUKINDO Alikuja USA miaka mingi iliyopita, inasemekana zaidi ya mika thelathini. Ameacha mke (African American) na watoto wanne, mkubwa alizaliwa 1989 familia yake haijui ndugu za Michael. Mazishi yatafanyika Jumamosi, ila mwili utachomwa. Kama unafununu au kujua lolote kuhusiana na ndugu yetu huyu unijulishe. Lengo nikuweza kuwafahamisha ndugu zake nyumbani Tanzania. 
Asante kwa ushirikiano wako.


Bariki Mwasaga 
bmwasaga@gmail.com