Friday, March 7, 2014

Je Wajua Kuhongwa kwa Mwanamke ni Haki yake Kutoka kwa Mwenyezi Mungu?


Kutokana na ugumu wa maisha wanaume tumegeuka kuwa walalamikaji linapofika suala la mpenzi wake kuwa very dependant sana kwako na badala yake tumewageuza na kuanza kuwaita majina(inferiority complex) kama vicheche,wachunaji,ruba hata muda mwingine kuwaita Malaya n.k
Na wao kwa kutokufahamu au kutokana na pressure kutoka kwa wanaume ya kuogopa kusemwa vibaya tumepachikwa majina na kuanza kuitwa Mabuzi,ATM n.k lakini ukweli wa mambo ulishawekwa/ulishapangwa bayana na Mkuu wa viumbe vyote,Muumbaji (Creator),Mwanasheria Mkuu,Mtabiri Mkuu Mwenyezimungu by the way dini zote uumbaji na mwanzo wa binadamu unatoa maelezo yanayofanana(katika andishi langu napenda nitumie reference ya biblia)
Mwenyezimungu aliitoa amri hii ukisoma Biblia GENESIS(MWANZO) aya 3:1-24 hapo ndipo utabiri na utaratibu wa miasha ya binadamu ,ulipangwa upya mara baada ya Hawa kushawishiwa na Nyoka(shetani) kula mti wa tunda la katikati naye akamgawia Adam ale pia , ndipo walipoanza kujua mema na mabaya katika bustani ya Eden
Nanukuu katika aya ya 3 mstari wa 16 GENESIS(mwanzo) 3:16 mwenyezimungu anatoa assignment/task “Akamwambia mwanamke hakika nitakuzidishia uchungu wako,na kuzaa kwako,kwa uchungu utazaa watoto na tamaa yako itakua kwa mumeo,naye atakutawala” -(kumbuka wenzetu hawajawahi kulalamika hata siku moja kuhusu kusaidiwa uchungu,kuzaa na tunawatawala they know its NATURE/amri kutoka kwa Mwenyezimungu)NB;mtawala siku zote ndo mpangaji wa mambo yote refer serikali katika suala la budget ,budget kama haitoshi/finyu wananchi watalalamika bila kujua fedha utapata vipi?

Ndipo anapomgeukia Mwanaume na kumpa adhabu/assignment-basic task(ambayo wengi wetu tunalalamika) yake Genesis(mwanzo) 3; 17-19 “akamwambia Adamu kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako ,ukala matunda ya mti ambao 
nilikukataza,ardhi imelaaniwa kwa ajili yako;kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako;18 michongoma na miiba itakuzalia nawe utakula mboga za kondeni 19;kwa jasho la uso wako utakula chakula hata utapoirudia ardhi ambayo katika hiyo ulitwaliwa”

Katika maelezo hayo hapo juu utagundua kuwa shughuli za ufanikishaji wa kimaisha ya binadamu(MAJUKUMU) katika ngazi ya familia zilishagawanywa(assigned) na Mwenyezimungu katika makundi mawili yaani ya kiuchumi ambayo alikabidhiwa mwanaume so we are responsible to provide Money,rent,shelter ,clothing and other expenses like shopping,Manicures,pedicures Voucher,M-pesa,Tigo-pesa etc na yale ya Uzazi kama kuzaa ,kutunza na kulea watoto wa 
familia alikabidhiwa mwanamke
Hivyo basi sio busara na ni kinyume na mafundisho ya imani ya dini mwanaume kulialia pale your girlfriend,wife,Mlupo etc anapodai haki yake ya kutunzwa na kukukumbusha umgharamie kwa sababu wewe ni mtawala wake tena unapaswa utii amri ya mwenyezimungu ambayo aliitoa Hapo MWANZO 3:1-24 ,Na hata upande wa UISLAM umeeleza bayana mwanamke akishaolewa hata kama anakazi she isn’t responsible katika gharama zozote za maisha(hata kuosha vyombo tu) labda aamue mwenyewe ,jukumu lake yeye ni uzazi na kulea(basic task zile…..)

Nawasilisha tulijadili ,changamoto zinakaribishwa pia

No comments:

Post a Comment