Saturday, April 12, 2014

RIYAMA: SIISHI MAISHA YA MAIGIZO

Superstar wa filamu za kibongo Riyama Ally,

MWIGIZAJI mwenye taito ya kujiheshimu, Riyama Ally, amefunguka kuwa kinachomfanya aishi vizuri na watu ni kwa sababu haishi maisha ya kuigiza.
Akizungumza na mwandishi wetu juu ya maisha yake, Riyama alifafanua:
“Mimi siangalii sana maisha ya anasa, naangalia zaidi masuala ya msingi ya jinsi ya kuishi na watu katika jamii na ndiyo maana unaona naishi maisha ya kawaida, siigizi hata kidogo, ukiigiza tu, unaumia.”