Friday, April 11, 2014

ALEX MSAMA ALAZWA HOSPITALI YA MKOA WA DODOMA NA HALI YAKE YAENDELEA KUWA NZURI MARA BAADA YA KUPATIWA MATIBABU

Baadhi ya Wakazi wa Mkoa wa Dodoma pamoja na Mwenyekiti wa Bongo Movie(Steve Nyerere) na Single Mtambalike wakiwa pembeni ya Mkurugenzi wa Msama Promotions Limited Bw Alex Msama kwaajili ya kumpa pole na kumfariji mara baada ya kupata ajali wakati akitokea Dar Es Salaam kuja Dodoma, ajali iliyotokea Ipagala Mwisho Kilometa chache tu kufika Dodoma Mjini.Picha na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog.
Na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog
Mkurugenzi wa Msama Promotion, Bw Alex Msama amepata ajali leo, eneo la Ipagala mwisho wakati akitoka Dar Es Salaam kuelekea Mkoani Dodoma, ajali hiyo imemuhusisha Dereva wa Bodaboda na gari la Bw Msama kugongana, Katika Ajali hiyo hakuna aliyepoteza maisha.
Akiongea na Mtandao wa Lukaza Blog, shuhuda ambae hakupenda jina lake kutajwa alisema "Gari la Bwa Msama lilikua likitoka Njia ya Morogoro Dodoma akielekea Dodoma Mjini wakati akiwa anaendesha gari, kuna bodaboda alikuwa akitokea Mjini Dodoma mara akaingia barabarani bila kuangalia mbele yake ndipo alipogongana na gari la Bw Msama"
Mara baada ya ajali hiyo kutokea Waliweza kukimbizwa katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwaajili ya kupata Matibabu zaidi. Baada ya kufikishwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma walipokelewa vizuri na kupelekwa chumba cha X-ray kwaajili ya kuangaliwa na mara baada ya kumalizika kwa vipimo vya X-ray waliweza kupelekwa Wodi namba moja kwaajili ya uangalizi wa madaktari na manesi.
Hali ya wagonjwa wote inaendelea kuwa nzuri mara baada ya kupatiwa matibabu ya haraka na kupatiwa vipimo. Wagonjwa wote wamelazwa Wodi namba 1 katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma.