Thursday, November 8, 2012
Wednesday, November 7, 2012
VODACOM WAKISHIRIKIANA NA BUSINESS PARTNER WAKE FTS SERVICES LTD WAWAPELEKA WATEJA WAO KISIWA CHA MBUDYA KILICHO BAHARI YA HINDI.
Hapa ndio Kisiwa cha Mbudya ambapo Vodacom imewapeleka wateja wake kwa ajili ya mapumziko ya week end jumamosi ya jana.
Wateja na wafanyakazi wa vodacom
Kushoto ni Steve Goyayi kutoka Stanbic Bank, wa tatu kutoka kushoto Asubisye Mwakatobe kutoka Vodacom na wengine ni baadhi ya wageni washiriki kutoka world Bank
Katikati ni Abdallah Singano kutoka Stanbic na kulia ni CEO wa MSD
Kutoka kushoto Steve Goyayi, Henry Kapinga na Abdallah Singano
Baadhi ya wafanyakazi kutoka Vodacom
Kushoto ni Idd Mbita Mkurugenzi wa FTS Services akiwa na Joseph Kusaga CEO wa Clouds FM na TV mwenye Tshirt ya kijani.
Wateja na wafanyakazi wa vodacom wakishuka kwenye boti maalum iliyokodiwa kwa ajili yao.
Kulia ni Henry Kapinga meneja mauzo wa FTS Services ltd akipiga picha ya kumbukumbu na CEO wa Clouds Joseph Kusaga
Wadau kutoka Vodacom wakipata vinywaji ndani ya kisiwa cha Mbudya
Rosalynn kutoka vodacom akiwashukuru wateja kwa kushiriki
Idd Mbita kutoka FTS Services akiwashukuru wateja kwa kushiriki na kuwaomba tudumishe ushirikiano wetu.
Vodacom Tanzania wakishirikiana na Business Partner wake FTS Services jana waliwapeleka wateja wao katika Kisiwa cha Mbudya kilicho katika bahari ya Hindi.
Tuesday, November 6, 2012
CCM NEW YORK STATE, CT AND MA
5 Novemba 2012
Kwa: Katibu Mkuu
Chama Cha Mapinduzi
Yahusu: Kumchagua tena Mwenyekiti wa Taifa Ndugu Dkt. Jakaya Kikwete
Kidumu Chama Cha Mapinduzi!
Kwa kauli moja Viongozi wa Tawi na Wanachama wote tunamuunga mkono Mwenyekiti Ndugu Dkt. Jakaya Kikwete kugombea nafasi ya Uwenyekiti wa Chama Taifa.
Ndugu Dkt. Kikwete ameonyesha umahiri, uongozi wenye tija na mafanikio katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Tunapenda kuungana na wanachama wote na wajumbe wa Mkutano Mkuu Dodoma kumchagua Mwenyekiti wetu Ndugu Mh. Jakaya Mrisho Kikwete
Kidumu Chama Cha Mapinduzi!
Ahsanteni
Katibu wa Tawi
Kny; Uongozi CCM New York
Monday, November 5, 2012
UZINDUZI WA MRADI WA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA GESI ASILIA KUTOKA MTWARA NA SONGOSONGO HADI DAR ES SALAAM

TAARIFA KWA UMMAWizara ya Nishati na Madini (MEM) inapenda kuutangazia umma kuwa Serikali inatarajia kuzindua mradi wa ujenzi wa miundombinu ya kusafisha na kusafirisha gesi asilia kutoka Mnazi Bay Mtwara na Songo Songo Kilwa hadi Dar es Salaam.
Hafla ya kuweka Jiwe la Msingi wa mradi huo itafanyika tarehe 8/11/2012 Kinyerezi, Manispaa ya Ilala, katika eneo ambapo mitambo ya kuendeshea mfumo mzima wa gesi itajengwa. Mgeni rasmi katika sherehe hiyo atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Wananchi wote wa Dar es Salaam na maeneo yanayozunguka eneo la Kinyerezi mnaalikwa na mnaombwa kufika kwenye eneo la mradi saa 2.00 asubuhi.
GESI ASILIA KWA MAENDELEO YA TAIFA
Imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini
TRAFIKI WAMPA KICHAPO MWANAJESHI MJINI MOSHI
MARA kwa mara jamii imekuwa ikisikia Wanajeshi wakiwapiga Askari wa Usalama barabarani hasa Jijini Dar es Salaam Trafiki wa Moshi huenda wamechoshwa na unyanyasaji huo kwa walinzi hawa wa amani na wasimamizi wa sheria amapo huko Mkoani Kilimanjaro, Askari wa kikosi cha usalama barabarani mjini Moshi ambao majina yao hayakufahamika wakimpiga askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) katika kiktuo kikuu cha mabasi mjini hapa hivi karibuni,baada ya kutokea kutoelewana,mwanajeshi huyo alikuwa akimtetea dereva wa Hiace aliyeshikwa na trafiki hao.//Picha na Nakajumo James.WATAKAOFELI KIDATO CHA PILI IMEKULA KWAO; WAZIRI
Dk Shukuru Kawambwa
WAKATI Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Pili ukianza leo nchini kote, Serikali imesema kuanzia sasa, mtihani huo utakuwa ni wa mchujo kuanzia sasa, hivyo atakayefeli atatimuliwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa alisema mtihani wa mwaka huu, matokeo yake yatatumika kama kigezo cha kuchuja na kukariri kidato cha pili kwa watahiniwa watakaoshindwa kufikia wastani wa ufaulu wa alama 30.
"Mtihani wa kidato cha pili kama ilivyo mitihani mingine ya taifa ni muhimu sana. Matokeo ya mtihani huu hutumiwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta) kama sehemu ya matokeo katika mtihani wa taifa wa elimu ya sekondari kidato cha nne," alisema Dk Kawambwa.
Alisema mtahiniwa ataruhusiwa kukariri kidato cha pili mara moja tu na endapo mtahiniwa atashindwa mtihani kwa mara ya pili kwa mwaka utakaofuatia, itabidi aendelee na elimu ya sekondari nje ya mfumo rasmi.
Dk Kawambwa alisema kurudishwa kwa mchujo katika mtihani huo ni moja ya njiia ya kuboresha elimu nchini na kupata wanafunzi walio bora nchini.
Alisema hayo ni mabadiliko ya kawaida na yataendelea kuwapo katika sekta hiyo kila mwaka
"Tunachopambania hapa ni ubora wa elimu nchini na hii itasaidia kuondoa wanafunzi wanaosemekana wanamaliza shule hawajui kusoma, japokuwa mimi siamini kama ni kweli," alisema Dk Kawambwa.
Alisema mtihani huo utamalizika Novemba 16, mwaka huu na idadi ya shule na vituo vilivyosajili watahiniwa mwaka huu ni 4,242 ikiwa ni ongezeko la vituo 55 ikilinganishwa na vile vilivyosajiliwa mwaka 2011 ambavyo vilikuwa 4,187.
"Kwa hiyo kwa mwaka huu kuna ongezeko la asilimia 1.3," alisema Dk Kawambwa
Alisema watahiniwa 442,925 wamejiandikisha kufanya mtihani. Kati yao wasichana ni 214,325 (sawa na asilimia 48.39) na wavulana ni 228,600 (sawa na asilimia 51.61).
"Wizara inaagiza wadau wote wa elimu katika kanda, manispaa na halmashauri za wilaya pamoja na wazazi kuhakikisha kuwa wanafunzi wote walioandikishwa kufanya mtihani wanafanya bila kukosa," alisema Dk Kawambwa.
Januari mwaka huu Serikali iliamua kurudisha mtihani huo kwa lengo la kupunguza matokeo mabaya ya kidato cha nne.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, alisema kuwa uamuzi wa Serikali wa kurudisha mtihani huo, umezingatia vigezo katika kuboresha matokeo ya kidato cha nne.
Mulugo alisema kuwa kuwapo kwa mtihani huo kutapunguza idadi ya wanaoshindwa kufaulu kidato cha nne.
“Kumekuwa na wanafunzi wazembe ambao wamefanya kupungua kwa idadi ya ufaulu kutokana na kukosekana kwa mtihani wa kidato cha pili, ambao ndiyo mwongozo wa mwanafunzi kufanya vizuri katika mitihani mbalimbali,” alisema Mulugo
.

Saturday, November 3, 2012
BRIGITTE ALFRED NDIE REDDS MISS TANZANIA 2012
Washereheshaji katika Onyesho la kumsaka Mlimbwende wa Redd's Miss Tanzania 2012 usiku huu ndani ya Ukumbi wa Hoteli ya Blue Peal,Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Taji Liundi na Kulia ni Jokate Mwegelo.
REDDS MISS TANZANIA 2012, BRIDGIT ALFRED (KATI) AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA MSHINDI WA PILI EUGENE FABIAN NA MSHINDI WA TATU EDA SYLVESTA (KULIA).
Warembo wa Redd's Miss Tanzania wakionyesha show yao mbele ya Watanzania katika Ukumbi wa Hoteli ya Blue Peal,Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam,usiku huu.
Warembo wakipita katika jukwaani na Mavazi ya Ubunifu.
Burudani ya Ngoma za Asili kutoka kwa Kundi la Wanne Star.
Wadau wa Miss Tanzania wakibadilishana Mawazo.
Wanahabari kazini.
Wadau kibao ndani ya Ukumbi wa Hoteli ya Blue Peal,Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam usiku huu.
Watu kibao ndani ya Ukumbi wa Hoteli ya Blue Peal,Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.
Wanalibeneke mzigoni kama kawaida.
NY TANZANIA COMMUNITY
Wanajumuiya!
Tunamshukuru M/Mungu kwa kuweza kuhimili dhoruba ya "Super storm Sandy". Pole sana kwa waliopoteza ndugu, jamaa na marafiki. Tunawashukuru sana Wanajumuiya kwa ushirikiano waliotoa kwa wanajumuiya waliohitaji msaada, kwa kutoa malazi na chakula na ukarimu mkubwa ambao hujawahi kutokea. Tuendelee na moyo huu. Tunafahamu itachukua muda kurudi katika hali ya kawaida, tafadhali wasiliana na jumuiya kama utahitaji msaada, tupo pamoja na wewe.
Bakia salama.
Shabani Mseba
The Secretary i.e
Friday, November 2, 2012
NEW YORK MARATHON CANCELED MAYOR BLOOMBERG SAY

Jonathan Sanger / NBC News
Runners and workers prepare for the New York City Marathon near Central Park in New York, N.Y. where generators were set up on Friday, November 2, 2012 to power a media tent.
By Andrew Mach and Elizabeth Chuck, NBC News
NEW YORK – The New York Marathon will not be held Sunday, Mayor Michael Bloomberg said Friday, backtracking just a few hours after he defended the decision to hold it despite heavy criticism as the city struggles back from Superstorm Sandy.
Thursday, November 1, 2012
Ommy Dimpoz Atangaza Kumsamehe Lord Eyez Kwa Kumwibia
Nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini Ommy Dimpoz amesema kuwa licha ya kutumia kiasi cha shilingi milioni 5 kurudisha gari yake kwenye hali ya kawaida hawezi kumchukia msanii mwenzake Lord Eyez anayeshikiliwa korokoroni hivi sasa kwa tuhuma za kuiba vifaa kutoka kwenye gari yake.
Akizungumza na mtandao huu mapema leo Ommy Dimpoz amefunguka kuwa ingawa kwa sasa haruhusiwi kusema lolote kuhusu jambo hilo lakini anayo haki ya kusema kuwa binafsi amesamehe na anamuachia Mungu.
“Nafahamu kuwa kuwa siruhusiwi kuzungumza lolote kwa kuwa suala liko Polisi,ninachoweza kukwambia ni kuwa binafsi nimemsamehe Lord na wenzake, sababu huwezi kujua kuhusu kesho, nimepanga kukutana naye na kumwambia hili jambo, najisikia vibaya lakini nashukuru kuwa gari yangu nimeshairekebisha na sasa ndiyo ninayoitumiatena licha ya kuwa nimetumiagharama kubwa” alisema Dimpoz.
Katika hatua nyingine nyota huyo wa songi la ‘Badae’ ameanika kuwa wimbo huo umemuingizia kiasi kikubwa cha pesa tofauti na yalivyokuwa matarajio yake huku pia akijikusanyia wingi wa marafiki ndani na nje ya nchi kupitia wimbo huo.
ARUSHA SASA KUITWA JIJI
ZISIKILIZE HAPA DAKIKA 30 ZA MASWALI KWA WAZIRI MKUU BUNGENI LEO NOV 1 2012.
Saa tatu kamili mpaka na nusu leo asubuhi Bungeni Dodoma 104.4 kulikua na kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri mkuu Mizengo Pinda ambapo pamoja na maswali aliyojibu ni kuhusu vigogo wa nchi kuwa na mamilioni ya pesa nje ya Tanzania, vurugu za kidini na mengine, msikilize hapo chini ambapo swali swali la kwanza liliulizwa na Mh Freeman Mbowe.
RAIS BARAKA OBAMA ATEMBELEA MAHENO YALIYO KUMBWA NA DHARUBA LA HURRICANE SANDY
Rais Baraka Obama akimfariji mmoja kati ya wahasirika wa hurricane sandy kwa kumpa warm hug katika ziara yake ya kutembelea maheneo yaliyo hasirika na hurricane sandy Uko New Jersey.

Hapa Rais Baraka Obama akiwa na Gov wa New Jersey Chris Christie punde tu baada ya kuwasiri uko New Jersey

Nyumba zilizo hasirika na hurricane uko New Jersey zimebakiwa tupu baada ya watu waliokuwa wanahishi umo ndani kukimbia makazi yao na kuziacha nyumba na mali zao ndani.

Daraja likiwa hoi bin taabani baada ya kuzidiwa na maji ya hurricane sandy na kusababisha mawasiria ya pande hizo mbili kuwa utata
Rais Baraka Obama akizungukia maheneo yaliyo kumbwa na dharuba hilo la hurricane kwa kutumia ndege ya kijeshi, hili kujionea maheneo yote yaliasirika na kutoa pole kwa wananchi wa maheneo hayo.
Subscribe to:
Posts (Atom)
















































