Kimgongomgongo asilia!!!
Monday, June 28, 2010
Wednesday, June 23, 2010
BUTI JIWE KUKAMUA MJINI EMMEN,HOLLAND
Jumamosi 26-06-2010
Mwanamziki Buti jiwe aka Henry Galinoma,Jr. mwenye maskani yake nchini Uholanzi anatarajiwa kutingisha jukwaa la onyesho kubwa la Midzomerhout Festival,mjini Emmen, huko Holand. Mwanamziki huyo wa mziki wa dansi wa afrika mashariki amechaguliwa kuwa ndiye mwanamziki pekee wa kiafrika nchini Uholanzi kuwakilisha katika onesho hilo, ambapo pia atawaongoza jukwaani wanamziki watakao kwenda na mwavuli wa jina la "Africa Breezze". Mwanamziki Buti Jiwe ameachia hewani album iliyobeba jina la "Samahani" ambayo inatamba katika vituo vingi vya redio ndani na nje ya Tanzania, hata hivyo Buti Jiwe ameahidi kuachia Remex ya album hiyo, kabla ya kumalizika mwaka 2010, hili kuhakikisha washabiki na wadau wa mziki wanapata mdundo wenye kuleta "Raha" katika burudani ya mziki.
Buti Jiwe amewaomba wadau na washabiki wa mziki walio ndani na nje ya Bongo kukaa mkao wa kula!! CD za Buti Jiwe zinahitaji pia msambazaji mzalendo, atakaye sambaza CDs katika nchi za afrika mashariki.
Tuesday, June 22, 2010
LEO KATIKA KUKUMBUKA SIKU YANGU NILIYOZALIWA, NINGEPENDA WATANZANIA WOTE NJE NA NDANI YA TANZANIA TUWAOMBEE VIONGOZI WETU WAPATE HEKIMA NA BUSARA YA KUTUONGOZA ILI NCHI YETU INEEMEKE KWA MAZURI.
TUWAOMBEE WAACHE "UBINAFSI", KWANI NDIO CHANZO CHA MATATIZO YETU MENGI NCHINI. NA TUWAOMBE WALIOSHINDWA UONGOZI WAACHIE!! WAKO WATANZANIA WENGI WENYE UWEZO MKUBWA WA KUWEZA KUIONGOZA NCHI, TENA WENYE MTAZAMO NA UPEO WA HALI YA JUU.
WATANZANIA WALIPA KODI NAWAOMBA MUONYESHE UCHUNGU NA PESA YENU KWA KUWA WADADISI NA NI NINI MNAFAIDIKA NA ULIPAJI WA KODI HIYO.
WATANZANIA MLIO NDANI NA NJE TUSIKUBALI TENA KUENDELEA KUWA "WANANCHI" BALI TUWE "WENYENCHI" KWA KUSHIRIKI KWENYE MAAMUZI MUHIMU NCHINI MWETU. TUWACHE KUTOA MALALAMIKO WAKATI SISI WENYEWE NDIYO TULIOWACHAGUA VIONGOZI WABOVU. UCHAGUZI UKO NJIANI NA TUNA HAKI YA KUTOMPA KURA ZETU YE YOTE AMBAE HAFAI.
TANZANIA TUNAWEZA KUPIGA HATUA KUBWA YA MAENDELEO KWA WATU WETU NA NCHI YETU. UONGOZI SIO "AWAMU" BALI NI DHAMANA.
NAMUOMBA MWENYEZI MUNGU ANIJALIE AFYA NJEMA NA MAISHA MAREFU NA NAMSHUKURU KWA HAPA ALIPOKWISHA NIFIKISHA!
MUNGU IBARIKI TANZANIA!!!!
Monday, June 21, 2010
Friday, June 18, 2010
KOBE NA LAKERS MABINGWA KWA MWAKA WA PILI MFULULIZO!!!
Katika mchezo ambao ulikuwa na kina aina ya ushindani kama itegemeavyo katika fainali za NBA, vijana wa Lakers waliweza kuwazihirishia wapenzi wao kwamba bado wao ni mabingwa kwa ushindi wa vikapu 83-79 dhidi ya washindani wao wa jadi Celtics na hivyo kuunyakua ubingwa kwa mwaka wa pili mfululizo.
Subscribe to:
Posts (Atom)