Friday, January 18, 2013

TRA, TUME YA UCHAGUZI NA JUMUIYA YA SERIKALI ZA MITAA (ALAT) WATOA MAONI KATIBA MPYA

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi akiwasilisha maoni ya Jumuiya hiyo kuhusu Katiba Mpya kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba jijini Dar es Salaam Ijumaa, jan 18, 2013. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Tume Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani.
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Ally saleh akiongea katika mkutano na Uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) uliokutana na Tume kuwasilisha maoni yake kuhusu Katiba Mpya katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Harry Kitillya (mwenye tai nyekundu) akiongea na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba mara baada ya Mamlaka hiyo kuwasilisha maoni yake kuhusu Katiba Mpya kwa Tume katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakiongozwa na Mwenyekiti wake Jaji Joseph Warioba (wa sita kutoka kushoto) katika picha ya pamoja na Viongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) waliongozwa na Mwenyekiti wa Bodiu ya TRA Bw. Bernard Mchomvu (wa nne kutoka kushoto) mara baada ya Mamlaka hiyo kuwasilisha maoni yake kuhusu Katiba Mpya jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment