Monday, August 26, 2013

WEMA SEPETU ADAIWA KUJIHUSISHA NA BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYA

Skendo ya mastaa mbalimbali Bongo kutajwa katika biashara na usafirishaji wa madawa ya kulevya ‘unga’ linazidi kuchukua sura mpya ambapo tayari majina ya wasanii wawili wakubwa, Wema Isaac Sepetu na Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’ yametajwa huku kinachowaponza kikijulikana.

Habari zinadai kuwa mastaa hao wameanza kujutia tambo zao za kutangaza utajiri walionao hivyo kuibua maswali kuwa huenda wana uhusiano na wafanyabiashara wa dawa za kulevya ikiaminika ndiyo njia ya haraka ya utajiri.

WEMA
Inadaiwa kuwa kitendo cha Wema kutangaza kununua nyumba, magari ya kifahari na kutapanya fedha ndiko kulikomponza na sasa anatajwa na wengi vinywani mwao juu ya kuhusika katika biashara hiyo haramu.

Kuna madai kuwa bosi huyo wa Endless Fame Productions amehojiwa juu ya suala hilo lakini meneja wake, Martin Kadinda alikanusha uvumi huo.

DIAMOND
Wiki iliyopita, Diamond aligeuka gumzo baada ya kuripotiwa akihusishwa na biashara hiyo huku ikidaiwa kuwa kinachomponza ni utajiri alioupata ghafla.

Ilidaiwa kuwa kitendo cha kutangaza kununua nyumba takriban tano jijini Dar, kumiliki kiasi cha Sh. bilioni moja kwenye akaunti na kuendesha magari ya kifahari ndivyo vilivyochangia watu kugeuzia antena za runinga zao kwake kutaka kujua ni matunda ya muziki tu au kuna kingine.

Madai ya jina la Diamond kutajwa katika saga hilo yalikwenda mbele zaidi ikielezwa kuwa kitendo cha kusafiri mara nyingi nje ya nchi huku akipiga picha na watu wanaosemekana kujihusisha na biashara hiyo nacho kilimponza.

Kwa upande wake, Diamond alisema kuwa hakuna mtu asiyejua namna anavyotafuta fedha kwa jasho juani hivyo watu wakimuona akila kivulini lazima wakumbuke kuwa amechumia juani na hajui chochote juu ya dawa hizo.