Sunday, September 15, 2013

TIMU YA SERIKALI KUWAHOJI AKINA MASOGANE JUU YA KESI ZA KUTUHUMIWA KUKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA NCHI ZA NJE

.MAPAMA jana Dar es salaam, Waziri wa nchi ofisi ya waziri Mkuu sera na uratibu wa shughuli za Bunge Wiliam Lukuvi alisema Serikali inafuatilia kwa karibu kesi zinazowahusisha Watanzania waliopo nje ya nchi wanaotuhumiwa na biashara ya dawa za kulevya wakiwemo wanamichezo na wasanii mbalimbali.

Alisema ilikuthibitisha hali hiyo timu ya watendaji imetumwa nchini Afrika kusini hivi karibu ili kukutana na kina Masogange kujua undani wa kesi yao na imethibitika kuhusika kweli na tuhuma hizo ambapo inasadikiwa jana kesi yao imesomwa rasmi na kusubiri hatua zaidi za kisheria.

Akizungumzia taarifa za kukamatwa kwa mwanamichezo Kaniki na Matumla, Lukuvi alisema taarifa hizo zitatolewa ufafanuzi zaidi na Serikali baada ya kupokea taarifa za kiofisi kutoka nchini Ethiopia.


Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha kupambana na kudhibiti na dawa za kulevya Godfrey Nzoa alisema kati ya timu waliokwenda Afrika kusini ni pamoja na yeye mwenyewe ambaye alifanikiwa kukaa kwa karibu na wafungwa hao akiwemo Masogange na kubaini kuna siri nzito mgongoni mwa Mwasogange hivyo inahitaji uchunguzi ili mkono wa sheria uweze kuwagusa wote wanaohusika na kutumia wasanii katika janga hilo.

“Ni kweli masogange na wenzie wamekamatwa na dawa aina za Ephedrine ambazo ndio zinazotengeneza dawa za kulevya na zinaruhusiwa kuingia nchi yeyote kwa kibali malaum kwani pia zinahusika kutengeneza dawa za kifua na timu iliyotumwa na Serikali imeweza kuzungumza nao lakini haimaanisha kwenda kwetu gerezani tunawatetea au tutawasaidia hapana kwakua hawakutumwa kufanya baisahara hiyo haramu ila tunajaribu kuwa karibu ili kuona wanapata haki zao na kuweza kubaini waliopo nyuma yao na kweli tumefanikiwa mnyororo ni mrefu tunaendelea na uchunguzi ili kujua wafadhili na mabosi zao tunawatiaje mikononi”alisema


Aliongeza kuwa ameshangazwa na kipato kidogo wanachopata wasanii hao akiwemo Masogange ambapo Afande Nzoa hakutaka kukiweka hadharani ili kupisha uchunguzi zaidi huku akiongeza kuwa kufuatia sheri iliyopo wasanii hao kesi zao zitafanyika Afrika kusini kwakua ndiko walikokamatiwa na endapo kuna mkataba wa ubadilishana wafungwa Serikali itaangalia njia ya kuwasaidia ili watumikie vifungo vyao nchini
Na jumamtanda

No comments:

Post a Comment