Thursday, January 16, 2014

SHOGA AWEKA HISTORIA BONGO

Stori: Imelda Mtema na Shani Ramadhani
KATIKA tukio linalochukuliwa kama ni la kihistoria kuwahi kutokea katika miaka ya karibuni, shoga wa Jijini Dar es Salaam, Amos Hamis, maarufu kama Anti Asu, aliyeokoka Agosti mwaka jana, ametangaza nia ya kutaka kuoa katika Kanisa la TAG, Magomeni wiki iliyopita.
Amos Hamis, maarufu kama Anti Asu akimvisha pete mpenzi wake.Amosi alimvalisha pete ya uchumba, Astrida Samatha baada ya kukamilisha taratibu zote za mila na desturi za ukweni na hatimaye kupewa ruksa ya kumuoa.

Mara baada ya misa ya pili kumalizika katika kanisa hilo, Amos alimvisha pete mchumba wake huyo na kusababisha nderemo na vifijo kutoka kwa waumini wa kanisa hilo, ambao waliahidi kuchangia baadhi ya gharama wakati wa harusi yao.
Anti Asu akipozi na mpenzi wake.Akizungumzia suala hilo, Amosi ambaye ni maarufu sana jijini Dar es Salaam enzi zake akijishughulisha na mapenzi ya jinsia moja, alisema:
"Siamini na wala sikuwahi kufikiria kama nitakuja kuwa na familia yangu, namshukuru sana baba mchungaji, kwani nina imani hata hao wanaoendelea na ushoga ipo siku watarejea kwa Bwana."
Anti Asu enzi zake.Amos alisema alijikuta akitamani kuwa na mwanamke baada ya kuokoka lakini hakuwa na mawazo hayo kipindi alipokuwa shoga.
Astrida, mwanamke aliye tayari kuolewa na Amos, alisema Mungu ameagiza upendo wa dhati ukiwemo ule wa roho, hasa kwa watu kama hawa na siyo vizuri kuwatenga.
"Tumeagizwa upendo ule wa roho, mimi naona ni sawa kwa kuwa na yeye ni mtu kama mimi na anahitaji upendo wa dhati na ninaahidi kumpenda," alisema Astrida.
Wapenzi hao wakiombewa.MCHUNGAJI ANENA 
Mchungaji kiongozi wa kanisa hilo, Dustan Kanamba, alisema Agosti, mwaka jana, Amos aliamua kuachana rasmi na ushoga na kuokoka, ndipo yeye na mke wake, walipoamua kumchukua na kuwa sehemu ya familia.
"Mimi na mke wangu tulishauriana na kumchukua ili awe mmoja kati ya familia yetu, japo kabla ya kuokoka alikuwa hajisikii kuwa na mwanamke lakini hali ilibadilika pale alipookoka na kujiona anahitaji kuwa na mwanamke kwani kwa kipindi cha miaka 29, Amos hakuwahi kumjua mwanamke," alisema mchungaji.
Anti Asu akimwinua kidole juu mchumba wake wakati akimvisha pete.WAUMINI WAMPONGEZA
Baadhi ya waumini wa kanisa hilo wamempongeza Amos kwa hatua aliyofikia na kuahidi kumpa sapoti katika ndoa yake inayotarajiwa kufungwa hivi karibuni, huku wakitaja baadhi ya vitu watakavyomuwezesha kama kumshonea suti ya kufungia ndoa na vinginevyo. 
Anti Asu akiwa kanisani na mchumba wake.Amos aliachana na mambo ya ushoga Agosti, mwaka jana baada ya kuokoka na kufanyiwa maombi na mchungaji kiongozi wa kanisa la T.A.G, Magomeni Mikumi jijini Dar. 
Anti Asu katika pozi lingine enzi zake.