Wednesday, July 29, 2009
WAPENZI WOTE WA BLOGU HII MNAKARIBISWA KUTUMA PICHA, MAKALA AU MAONI KWA KUPITIA BARUA-PEPE: www.fundikramadhani@cs.com
-KARIBUNI-
Tuesday, July 28, 2009
Monday, July 27, 2009
MAMBO YA BONGO
Nilipokuwa kwenye likizo yangu niliona mambo/vitu ambavyo vimenifanya nijiulize maswali mengi bila kuwa na majibu.
1. Nilishangazwa sana na jinsi sehemu za starehe(mabaa) wanavyofurika watu katika siku zote za juma(Jumatatu mpaka Jumatatu). Je! hii ina maana ya kwamba uwezo wa watu kifedha ni mkubwa sana au pengine tumegeuka kuwa Taifa la walevi? Au pengine starehe ndio shughuli yetu kubwa na muhimu kuliko kitu kingine. Tukumbuke ya kuwa mtindo huu vile vile unaandamana na mambo mengi yanayochangia kwenye kuiangamiza jamii na kurudisha au kuchelewesha maendeleo ya kweli.
2. Nilishangazwa na jinsi makampuni ya simu yalivyotanda na mabango yao ya matangazo karibu kila sehemu, lakini ni mara chache unaweza ukakutana na mabango ya kutukumbusha kuhusu ukimwi kama vile sio tatizo tena Tanzania.
3. Uongozi wa serikali na chama katika Jiji la Tanga umezorota na unachangia sana katika kukwamisha maendeleo ya Jiji hilo(ambalo hata hadhi ya kuitwa Jiji halina). Waarabu wa Tanga si wapenda maendeleo, na ndugu zangu wa Kidigo itatubidi tuchangamke kama tunataka maendeleo.
4. Wanaoiba si kwamba wanaiibia serikali bali ni sisi sote hivyo tusikubali...
Kwa ndugu zangu mlio nje ya nchi yetu tukufu kwa kipindi kirefu ni vizuri tukakumbushana jinsi fedha yetu ya madafu inavyofanana. Kwani kuanzia uhuru mpaka wa leo imeshabadilishwa mara nyingi tu, na si ajabu siku utakayoamua kurudi ukakutana na mjanja atakayetaka kukubambiza na zile zisizotumika tena.
Saturday, July 25, 2009
Tuesday, July 21, 2009
Mwanamziki Ras Makunja aka Bw.Kichwa Ngumu na mzimu wake FFU ,juzi jumamosi walifungua ukurasa mpya katika jukwaa la Fest-Africa,kwani waliweza kuwapa burudani ya aina washabiki wa ufini,
wanamziki washambuliaji (FFU) wa safu ya mbele waliweza kuwamdudu washabiki vizuri,Ras Makunja kiwaongoza jukwaani washambuliaji wake wa safu ya mbele mpiga solo Chris-B,ambaye pia anaimba na Bi.Severne aka Sevasha au afande wa kike,huku mdundo mkali wa The Ngoma Africa Band ukiwasindikiza na kuweza kufanikiwa kuwayumbisha washabiki katika onyesho hilo!
Kitu cha kufurahisha mziki huo wa Ngoma Africa uliweza kuwazoa washabiki na kupanda jukwaani kusakata ngoma za moto! mojawapo ya walivutwa jukwaa ni "Mzee Mponda" au tumwite "Dady Mponda" alipanda jukwaani na akawashangaza maelfu ya washabiki kuwa "kuwa wazee wa Kiafrika" wanajua kucheza mziki na kutoa ushindani kwa vijana!
wasikilize ngoma afrika hapa http://www.myspace.com/thengomaafrica

Subscribe to:
Posts (Atom)