Monday, April 14, 2014
NICKI MINAJ SHOW OFF HER BUMP TO BUMP

Someone's pleased with themselves: The chart topper also posted a collage showing her from multiple angles

Darling Nicki: She certainly seemed to know what she was doing as she struck a sexy pose in her car's backseat

That's more like it: The rapper is best known for her outrageously revealing performance outfits
Sunday, April 13, 2014
JK ATEMBELEA MAENEO YALIYOKUMBWA NA MAFURIKO MKOA WA PWANI
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali mmoja wa baadhi ya abiria waliokwama baada ya barabara ya Chalinze-Dar es Salaam kuharibiwa vibaya na mafuriko
.jpg)
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Mkewe Mama Salma Kikwete na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza wakikagua athari za mafuriko zilizoharibu vibaya barabara ya Chalinze- Dar es Salaam eneo la Ruvu Darajani leo.Mamia ya abiria walikuwa wamekwama kutokana na mafuriko hayo
.jpg)
.jpg)
Rais akisalimiana na mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Bwawani iliyopo Mkoani Pwani wakati alipotembelea eneo la Ruvu lililoathiriwa na mafuriko leo.
.jpg)
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Mke wa Rais Mama Salma Kikwete,Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza na Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete wakikagua athari za mafuriko maeneo ya Ruvu Darajani na Visiga
Picha na Freddy Maro.
TAARIFA KAMILI YA AJALI YA HELKOPTA ILIYOMBEBA MAKAMU WA RAIS NA MAAFISA WENGINE WA SERIKALI
Helikopta waliyokua wakisafiria Makamu wa Rais Dr. Gharib Bilal, waziri wa ujenzi John Magufuli, Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadick imepata ajali asubuhi wakati ikipaa kutoka uwanja wa ndege Dar es salaam. (kwa mujibu wa mashuhuda)
Taarifa zilizotoka muda mfupi baadae zimeeleza kupata majeruhi lakini hakuna yeyote aliepoteza maisha baada ya Helikopta hiyo kuanguka wakati ikianza safari kuwapeleka viongozi hao kutembelea maeneo yaliyoathirika na mafuriko.
Wote walitoka salama na majeraha madogomadogo ambapo pia kwenye taarifa nyingine iliyotolewa na TBC, wameendelea na ziara ya kutazama athari za maafuriko kwenye sehemu mbalimbali ikiwemo Pwani.
Ajali hii ya Helikopta imetokea siku moja baada ya ndege ya shirika la ndege la Kenya kubamiza chini na kuharibu upande wa kulia wa bawa kutokana na ukungu mkubwa uliokuwepo kwenye uwanja wa ndege Dar es salaam wakati ikitua kutokea Nairobi, hakuna aliepoteza maisha ila waliojeruhiwa wakati wa kushuka kwa dharura kutoka kwenye ndege.
Taarifa kutoka kwa mmoja wa Waliokuwemo kwenye Helikopta hii ya jeshi inasema wakati inapaa kwenye umbali wa kama futi tano hivi kutoka uwanja wa ndege Dar es salaam, ilizidiwa na upepo ulioirudisha nyuma na kuangukia paa kabla ya kutua chini.

Kilichofanyika ni watu waliokuwemo kutoka nje harakaharaka kisha aliekua akiiendesha kufungua tenki la mafuta na kumwaga mafuta yote alafu baada ya muda mfupi vikosi vya zimamoto vikaanza kuipiga maji helikopta hiyo ili kuepusha mlipuko.
Unaambiwa kama ingekua ni majira ya moto, helikopta hii ambayo ilikua inawapeleka kutazama maafuriko yaliyookana na mvua Dar es salaam ingeweza kuwa kwenye hatari zaidi ya kulipuka.
Saturday, April 12, 2014
RIYAMA: SIISHI MAISHA YA MAIGIZO
Superstar wa filamu za kibongo Riyama Ally,
MWIGIZAJI mwenye taito ya kujiheshimu, Riyama Ally, amefunguka kuwa kinachomfanya aishi vizuri na watu ni kwa sababu haishi maisha ya kuigiza.
Akizungumza na mwandishi wetu juu ya maisha yake, Riyama alifafanua:
“Mimi siangalii sana maisha ya anasa, naangalia zaidi masuala ya msingi ya jinsi ya kuishi na watu katika jamii na ndiyo maana unaona naishi maisha ya kawaida, siigizi hata kidogo, ukiigiza tu, unaumia.”
Friday, April 11, 2014
ALEX MSAMA ALAZWA HOSPITALI YA MKOA WA DODOMA NA HALI YAKE YAENDELEA KUWA NZURI MARA BAADA YA KUPATIWA MATIBABU
Baadhi ya Wakazi wa Mkoa wa Dodoma pamoja na Mwenyekiti wa Bongo Movie(Steve Nyerere) na Single Mtambalike wakiwa pembeni ya Mkurugenzi wa Msama Promotions Limited Bw Alex Msama kwaajili ya kumpa pole na kumfariji mara baada ya kupata ajali wakati akitokea Dar Es Salaam kuja Dodoma, ajali iliyotokea Ipagala Mwisho Kilometa chache tu kufika Dodoma Mjini.Picha na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog.
Na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog
Mkurugenzi wa Msama Promotion, Bw Alex Msama amepata ajali leo, eneo la Ipagala mwisho wakati akitoka Dar Es Salaam kuelekea Mkoani Dodoma, ajali hiyo imemuhusisha Dereva wa Bodaboda na gari la Bw Msama kugongana, Katika Ajali hiyo hakuna aliyepoteza maisha.
Akiongea na Mtandao wa Lukaza Blog, shuhuda ambae hakupenda jina lake kutajwa alisema "Gari la Bwa Msama lilikua likitoka Njia ya Morogoro Dodoma akielekea Dodoma Mjini wakati akiwa anaendesha gari, kuna bodaboda alikuwa akitokea Mjini Dodoma mara akaingia barabarani bila kuangalia mbele yake ndipo alipogongana na gari la Bw Msama"
Mara baada ya ajali hiyo kutokea Waliweza kukimbizwa katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwaajili ya kupata Matibabu zaidi. Baada ya kufikishwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma walipokelewa vizuri na kupelekwa chumba cha X-ray kwaajili ya kuangaliwa na mara baada ya kumalizika kwa vipimo vya X-ray waliweza kupelekwa Wodi namba moja kwaajili ya uangalizi wa madaktari na manesi.
Hali ya wagonjwa wote inaendelea kuwa nzuri mara baada ya kupatiwa matibabu ya haraka na kupatiwa vipimo. Wagonjwa wote wamelazwa Wodi namba 1 katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma.
Thursday, April 10, 2014
SIMULIZI TAMU YA WEMA SEPETU-5
Wema Sepetu 'Madam'.
VIPI KUHUSU HARTMANN?
Mwandishi: Iliwahi kusemekana kuwa kuna wakati uliangukia kwenye penzi la mjasiriamali anaitwa Hartmann Mbilinyi, ni kweli?
Wema: Yale yalikuwa maneno ya watu. Unajua Hartmann nilikuwa nafanya naye kazi za filamu, wakati ule alikuwa na kampuni yake inaitwa Hartmann Production, watu wakadhani ‘nadate’ naye, si kweli bwana.
Mwandishi: Wema unaweza kutuambia mwanaume gani alifuata baada ya wewe kuachana na Diamond akawa na Jokate?
Sasa endelea….
Wema: Baada ya Diamond nilipenda sana kuishi mwenyewe kwani sikuwa na hamu ya kuwa na mpenzi. Nilichoshwa sana.
AKUMBUKA MACHUNGU YA DIAMOND KUKATAA KUPOKEA FEDHA ZAKE JUKWAANI
Mwandishi: Kuna mwaka uliwahi kuhudhuria shoo ya Diamond pale Mlimani City, tayari akiwa na Jokate rasmi, ukaenda kumtuza pesa jukwaani akazikataa, ulijisikiaje?
Wema: Sitaki kukumbuka. Ilikuwa mbaya sana. Unajua nilikwenda kama shabiki lakini yeye akachukulia vingine, iliniuma sana. Lakini nilisema yote maisha.
“Nisingeweza kumfuata Diamond kwa lengo lingine wakati najua alikuwa na Jokate.
“Hata nilipofika nyumbani bado akili zangu zilikuwa zikirudia lile tukio mara kwa mara. Hapo ujue ni jinsi gani niliumia ila nasema na watu wajue kwamba sikwenda kwa nia nyingine zaidi ya kutuza kama mashabiki wengine tu.
“Kuna watu walinishauri kwamba ningefanya fujo palepale ukumbini lakini hilo nililiona ni wazo baya, Diamond hakujua kwamba napenda muziki wake hata kama yeye tuliachana akawa na Jokate.
“Jokate mwenyewe kwa sasa tupo sawa kabisa, tulikutana Arusha tukayaongea, anajua kwa sasa nimerudiana na Diamond, imebidi akubali matokeo kama mimi nilivyo yakubali matokeo wakati ule.”
KUHUSU KIGOGO WA IKULU
Mwandishi: Vipi ukajikuta umeangukia kwa Clement wa Ikulu?
Wema: Yule alikuja baada ya kuwa singo. Nilimkubali kwa sababu kwa wakati ule sikuona kipingamizi cha mimi na yeye kuwa wote, ni mwanaume anayejua kulea, kupenda.
Mwandishi: Ulijua ni mume wa mtu wakati mnaanzana?
Wema: Hapana, lakini nadhani kwa sababu hatukulizungumzia hilo zaidi ya uhusiano wangu na wake. Na alijua nilikuwa na Diamond, tukaachana.
Mwandishi: Unaweza kueleza kidogo maisha yenu ya kimapenzi?
Wema: Kwa yule tuachane naye.
Mwandishi: Kwa nini mliachana?
Wema: Ilitokea, ikawa hivyo.
Mwandishi: Inadaiwa yeye ndiye aliyekupangia ile nyumba na kukununulia kila kitu cha ndani, ni kweli?
Wema: Nasisitiza yule tumwache.
Mwandishi: Ni kweli ni mfanyakazi wa Ikulu?
Wema: (akionesha kukasirika) lakini si nimeshasema yule tumwache, mbona bado unaniuliza maswali kuhusu yeye au unapenda tufikie mwisho wa mahojiano yetu?
Mwandishi: Oke, kuna siku za furaha na siku za majonzi. Ni siku gani iliwahi kuwa ya furaha kwako na majonzi?
Wema: Siku Diamond aliponivisha pete ya uchumba pale Maisha Club. Nililia kwa furaha.
“Siku ambayo nilikosa furaha ikawa ya majonzi ni pale baba yangu mzazi (marehemu Isaac Sepetu) alipofariki dunia.”
KUHUSU MKOROGO
Mwandishi: Wema umekuwa ukidai mkorogo uliharibu ngozi yako, ukatumia fedha nyingi kurekebisha ngozi. Lakini mbona upo vilevile?
Wema: Hapana, mimi ndiyo najijua, nilivyokuwa kabla na sasa. Ngozi yangu iliharibika sana kwa sasa iko sawa kabisa na sirudii tena kutumia mkorogo.
KURUDIANA NA DIAMOND KULIVYOTOKEA
Mwandishi: Sasa ilikuwaje ukarudiana na Diamond?
Itaendelea wiki ijayo.
TAARIFA NA LUGHA SAHIHI: DHANA YA KUPUNGUZA MADHARA YA MAAFA
Meneja wa kituo cha Kahama FM Redio, Marco Mipawa, akiwakaribisha washiriki na kufungua warsha ya mafunzo ya siku nne ya waandishi wa habari na watangazaji wa Redio Jamii kuhusu kuandika taarifa za Maafa na Misaada ya Kibinadamu yanayofanyika mjini Kahama. Kushoto ni Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO Mama Rose Haji Mwalimu na kulia ni Hellen Msemo kutoka Mamamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA).
Na Mwandishi Wetu
Ukosefu wa taarifa na lugha sahihi halikadhalika kukosa uelewa katika jamii ni miongoni mwa mambo yanayosababisha kutokea kwa maafa.
Katika mada inayohusu Misaada ya Kibinadamu na Taarifa za Maafa katika mafunzo ya siku nne ya wanahabari na watangazaji wa redio jamii mjini Kahama Mratibu wa idara ya Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bwana Harrison Christopher Chinyuka alisema jamii lazima ifahamu historia ya maeneo yanapotokea maafa na wapate elimu ya kutosha ili waweze kuepusha maafa asili.
Bwana Chinyuka alisema kwamba hilo litafanikiwa iwapo waandishi wa habari watawajibika kikamilifu kwa kuandika taarifa za majanga na maafa ambazo ni sahihi na kwa wakati kwa sababu wakati mwingine wamekuwa wakishindwa kutumia lugha sahihi ya kusheheneza taarifa husika.
Mratibu wa Idara ya Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bwana Harrison Christopher Chinyuka Chinyuka, akiendesha mafunzo kwa waandishi na watangazaji wa Redio za Jamii nchini.
“Wanahabari wana mchango mkubwa katika kuhakikisha kuwa madhara ya maafa yanapunguzwa kwa kuipa uelewa jamii husika kwa kutoa taarifa na lugha sahihi zinazohusu maafa ili kutoa nafasi kwa wahanga kujihami ipasavyo”, alisema Bwana Chinyuka.
Wajibu wa mwandishi wa habari katika kupunguza maafa ni kukuza uelewa wa jamii kuhusu hatua za hatari, kuzuia na kukabiliana na maafa, kukubaliana juu ya viwango vya taratibu za uendeshaji katika sehemu ya maafa.
Wajibu mwingine ni kusambaza ujumbe wa onyo kwa kuaminika na haraka iwezekanavyo na kuiweka jamii vizuri kitaarifa wakati huo huo kuepuka uvumi na hofu katika hali ya hadhari.
Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO Mama Rose Haji Mwalimu, akihamaisha washiriki katika vikundi kazi.
“Wajibu wenu waandishi wa habari kabla, wakati na baada ya maafa ni kutimiza jukumu la kulinda na kusaidia kuunganisha familia na kujenga kujiamini, sio kuachia mchakato njiani”, alisema Bwana Chinyuka.
Madhumuni ya mafunzo hayo ni kutoa uwezo kwa waandishi wa habari na watangazaji wa redio jamii kuandika taarifa zinazohusu kutoa msaada wa kibinadamu na kupunguza madhara yatokanayo na majanga na maafa nchini katika mradi unofadhiliwa na shirika la maendeleo ya Sweden (SIDA) kwa kushirikiana na UNESCO.
Mafunzo hayo yanatekeleza malengo ya UNESCO linalohusisha kuimarisha uwezo wa kukuza mazingira ya uhuru wa kujieleza kwa ajili ya maendeleo, kuendeleza demokrasia na utamaduni wa mazungumzo ya amani bila migogoro.
Hellen Msemo kutoka Mamamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), akifafanua jambo wakati wa mafunzo hayo.
Mwandishi na mtangazaji kutoka kituo cha Redio O.R.S FM ya Simanjiro, Julius Laizer, akichangia maoni wakati wa mafunzo hayo yaliyofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) kwa kushirikiana na UNESCO.
Picha juu na chini ni sehemu ya washiriki wakifuatilia mafunzo hayo kwa umakini yaliyofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) kwa kushirikiana na UNESCO.
Mafunzo yakiendelea.
Tuesday, April 8, 2014
BABA DIAMOND "MWANANGU SI RIDHIKI YANGU...HANISAIDII KITU"
Baba Mzazi wa Mwanamuziki Maarufu na Mwenye Pesa nyingi Kutokana na Mziki Kuliko Wanamuziki Wote Bongo Diamond Amefunguka na Kuliambia Gazeti Moja hapa Bongo Kuwa Mwanamuziki huyu Si Ridhiki Kwake kwani Hamjali wala kumsaidia kama Baba yake ...Mpaka Leo haijulikani kwanini Diamond hamkubali huyu jamaa kama baba yake...Mapenzi yote amehamishia kwa mama yake ambae ndio aliyemleta toka akiwa mdogo......Diamond Msamehe Mzee Hata kama alikutosa ukiwa Mdogo......!!
MAJAMBAZI WATEKA MAGARI YA MAGAZETI,GARI LA MWANANCHI LAPINDUKA.. DEREVA MMOJA ATESWA, .!!!
Madereva wa gari la magazeti ya kampuni ya The Guardian Rashid Yusuph Kahese (37) kushoto na mwenzake Ally Malinda (44) ambao wamenusurika katika utekaji huo.
Gari la magazeti la kampuni ya The Guardian ambalo limetua Iringa hivi sasa saa 2.40 Asubuhi hii baada ya kupona kutekwa
MAJAMBAZI ambayo idadi yao haikufaanika mara moja usiku wa leo wamefunga barabara ya Morogoro -Iringa eneo la Doma na kufanya unyama wa kutisha kwa wasafiri wa barabara hiyo ikiwa ni pamoja na kuwalazimisha kufanya mapenzi wanaume kwa wanaume na kuwatesa vibaya madereva kabla ya kuwapora mali zao.
Miongoni mwa walioteswa na pamoja na rasta dereva wa gari la magazeti ya kampuni ya globalpublishers ambae anadaiwa kujeruhiwa mkono wake huku dereva wa gari la magazeti ya kampuni ya Mwananchi akinusurika na gari lake kupinduka wakati akikwepa vizuizi vya magogo vilivyotegwa barabarani.
Wakizungumza asubuhi ya leo mjini Iringa wahanga wa tukio hilo Ally Malinda (44) mkazi wa Itunda Dar es Salaam na Rashid Yusuph Kahese (37) mkazi wa Mbezi jijini Dar es Salaam ambao kwa pamoja wanaendesha gari ya magazeti ya kampuni ya The Guardian walisema kuwa tukio hilo lilmetokea mida ya saa 8 usiku wa leo hadi saa 11 Alfajiri baada ya watekaji hao kuachia mateka hao.
Malinda alisema kuwa kabla ya kufika eneo ambalo watekaji hao walikuwa wamewateka abiria wengi zaidi walikutana na makundi ya watu waliotekwa na kuporwa ambao walikuwa wakiwasimamisha wasiendelee na safari ila hawakusimama wakijua ni wezi
"Tulienda mbele kidogo tukakutana na kundi jingine ila bado tulipuuza na kupita baada ya kufika mbele ndipo tuliona magari yakiwa yamegeuka huku na kule huku wengine wakiteswa na ndipo tulipofanikiwa kugeuza gari letu lenye namba za usajili T 812 CNZ na kukimbia.
Hata hivyo alisema polisi Morogoro walipigiwa simu ila hawakuweza kufika hadi majira ya saa 11 Alfajiri watekaji hao walipoamua kuwaachia mateka.
"Kila tukimpigia kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro aliishia kusema kuna askari wametumwa kuja eneo la tukio ila hadi asubuhi hakuna askari aliyefika .....na majeruhi wamepelekwa Hospital ya mkoa wa Morogoro kwa matibabu zaidi"
Mtandao huu unaendelea kumtafuta kamanda wa polisi wa mkoa wa Morogoro ili kuzungumzia tukio hilo zaidi.
Monday, April 7, 2014
NY EBRA BIRTHDAY PARTY CHECK OUT HERE
Ny Ebra akipakwa cake usoni na Farida kutoka CT, Birthday party hiyo ilifanyanyika nyumbani kwa Ny Ebra na kurushwa moja kwa moja live stream na Vijimambiotv and Radio. Marafiki waliofika kwenye party hiyo walipata chakula vinywaji na muziki mzuri kutoka kwa (DJ Luke Joe) kutoka DC, DjLuke kwa upendo alionao kwa mdogo wake alisafiri kutoka DC hadi New York kwenda kusababisha nyumba ya machine.Ny Ebra anatanguliza shukran zake za thati kwa watu waliofanikisha party hii ni Seif Akida (Big brother), Deo Mhella, Sadik Ally, Na kwa upande wa akina dada ni Adella, Asha, Brenda na Flora. Shukrani kwa wote waliofika na show love na kwa wale walioshindwa kutokea Ny Ebra anawajari na kuwapenda daima.
Mahesabu ya kukata cake hayo kisu kikubwa utadhania panga ...
Seif Akida pembeni akisimamia ukataji cake na upande wa kushoto ni Seif na Bob ni masuper star wa The Calturel Wars Movie inayotarajiwa kutoka muda wowote ....
Dada wa Ny Ebra Adella akipeleka cake mezani
Ebra akimrisha dada yake cake na pembeni anaengaa sharubu ni rafiki wa Ebra Arifah kutoka New Jersey.
Subscribe to:
Posts (Atom)