Friday, June 26, 2009

Mr. Hashim T. akichekelea baada ya kuchaguliwa namba mbili kwenda kuchezea timu ya Memphis wakati wa uchaguzi wa mwaka huu wa kuingia NBA... WABONGO WOTE TUNAKUPA HONGERA NA KUKUTAKIA MAFANIKIO MAKUBWA! Wakilisha..


LOS ANGELES – Authorities are seeking to clear up the mystery surrounding Michael Jackson's death, including whether prescription drugs could have been a factor.
An autopsy was planned for Friday, though results weren't likely to be final until toxicology tests could be completed, a process that could take several days and sometimes weeks. However, if a cause can be determined by the autopsy, they will announce the results, said Los Angeles County Coroner Investigator Jerry McKibben.
Police said they were investigating, standard procedure in high-profile cases.
Brian Oxman, a former attorney of Jackson's and a family friend, said he was concerned about Jackson's use of painkillers and he warned the singer's family about possible abuse.
"I said one day, we're going to have this experience. And when Anna Nicole Smith passed away, I said we cannot have this kind of thing with Michael Jackson," Oxman said Friday on NBC's "Today" show. "The result was, I warned everyone, and lo and behold, here we are. I don't know what caused his death. But I feared this day, and here we are."
The 50-year-old musical superstar died Thursday, just as he was preparing for a series of 50 concerts starting July 13 at London's 02 arena.
He died at UCLA Medical Center after being stricken at his rented home in the posh Los Angeles neighborhood of Holmby Hills. Paramedics tried to resuscitate him for nearly three-quarters of an hour, then rushed him to the hospital, where doctors continued to work on him.
His brother Jermaine said it was believed that Jackson suffered cardiac arrest at his home. Cardiac arrest is an abnormal heart rhythm that stops the heart from pumping blood to the body. It can occur after a heart attack or be caused by other heart problems.
A handful of bleary-eyed fans camped out throughout the night with media outside the Jackson family house in the San Fernando Valley and near his star on the Hollywood Walk of Fame.
Oxman, who said he was speaking on behalf of no one but himself, and other friends made the rounds among the news outlets, adding to the intrigue of Jackson's early demise. Oxman claims Jackson had prescription drugs at his disposal to help with pain suffered when he broke his leg after he fell off a stage and for broken vertebrae in his back.
"When the autopsy comes, all hell's going to break loose, so thank God we're celebrating him now," Liza Minnelli told CBS' "The Early Show" by telephone.
In 2007, Jackson settled a lawsuit filed by a Beverly Hills pharmacy that claimed the singer owed more than $100,000 for prescription drugs over a two-year period.
After Jackson was acquitted on child molestation charges in 2005, Santa Barbara County District Attorney Tom Sneddon argued returning some items belonging to Jackson he labeled "contraband." Sneddon said those included syringes, the drug Demerol and prescriptions for various drugs, mainly antibiotics, that were in different people's names.
Jackson's 1982 album, "Thriller," is the best-selling album of all time, with an estimated 50 million copies sold worldwide.
Billboard magazine editorial director Bill Werde said Jackson's 13 No. 1 one hits on the Billboard charts put him behind only Elvis Presley, the Beatles and Mariah Carey.

Thursday, June 25, 2009












Afrika ya Kusini yalala bao 1-0 kwa Wabrazili... wachawi wa soka!










LOS ANGELES – Michael Jackson's brother says it's believed that the pop star died of cardiac arrest.
Jermaine Jackson cautioned at a hospital press conference Thursday that the cause of his death would not be known until an autopsy was performed.
He said Michael Jackson's personal doctor and paramedics tried to resuscitate him at his rented home in Holmby Hills. A team of doctors at UCLA Medical Center also tried for more than an hour.
Los Angeles police Lt. Gregg Strenk said at a separate news conference that police robbery-homicide detectives have been ordered to investigate, which is common in a high-profile case. Strenk says the coroner's office, which will handle inquiries into the type of death, is taking possession of the body.





Tuesday, June 23, 2009

Nani alisema eti ghorofa lazima ijengwe kwa tofali na vyuma na sio udongo na miti?


Raisi wa kwanza wa majirani zetu - Mzee Jomo Kenyatta.
Mzee alikuwa anakizungumza sana kiswahili na alikuwa mtani sana. Watu walipokuwa wanamuita Mzee, yeye aliwajibu kiutani kwamba "mimi sio Muzee na kama uhamini muulize mama Ngina". Huyu ni shujaa mwingine mkubwa wa Afrika.


Hivi ndivyo ilivyokuwa wakati Waitaliano walipopambana na Wabrazili huko kwa Bwana J. Zuma

Friday, June 19, 2009

Wednesday, June 17, 2009








Ilikuwa ni patamshika leo siku ya Jumatano, June 17, 2009 wakati timu ya Taifa ya Afrika ya Kusini ilipopambana na timu ya Taifa ya New Zealand wakati wa mchuano wa Confederations Cup kundi la A katika uwanja wa Royal Bafokeng mjini Rastenburg, Afrika ya Kusini. Katika picha za juu, anaonekana mchezaji Steven Pienaar wa Afrika ya Kusini akiminyana na Wanew Zealand.












Mashabiki wa Bafana Bafana wakiishabikia timu yao leo wakati wa mechi na New Zealand.











---------------------------------------------------------------------------


Wasomaji, naanza na BAPisms:

Ø
Maisha bora hayanyeshi kama mvua; sio tukio (event)! Maisha bora ni mchecheto (process) yanatokea baada ya muda (over time).

Ø Wakati mwingine ni vigumu kuwabadilisha walalahoi wetu; inabidi twende pole pole na baadhi ya walalahoi wetu wanaolegalega (the laggards) ili tufanikiwe kuwavusha.

Ø Wa-Barbaig ni wa-Tanzania wetu; tuwatoe kutoka hizo nyumba zao za jadi hadi kwenye nyumba za kisasa zenye matofali ya udongo na kuezekwa kwa nyasi.

Ø Tunaweza kuboresha nyumba za tembe za wa-Gogo za asilia (nyumba zinazolinga na mazingira) kwa kuziwekea madirisha na milango ya kisasa hata kuwa nyumba za maghorofa-tembe!

Ø Tuwavushe wa-Jita wangu wote kutoka hizo nyumba zao za udongo zisizo na madirisha (eti, wanaogopa wachawi watawachungulia usiku.)

Ø “Nyumba bora sio lazima ijengwe kwa matofali ya kuchoma na kuezekwa kwa bati. Kuna magofu ya majumba ya zamani yaliyozagaa kwenye “amatongo” (mahame) huko kwetu (Majita, Musoma) yaliyojengwa kwa matofali mabichi ambayo bado yamesimama baada ya kuwa “oxidized” na jua!

Ø Magofu ya namna hiyo (adobe houses) pia yapo sehemu za mikoa ya Arizona na New Mexico hapa Amerika ya wazawa wa nchi hii.

BAPisms hizo zinatokana na Maggid Mjengwa kuweka kwenye blog yake (mjengwa.blogspot.com) picha yenye kichwa, “Maisha Haya ' SI MCHEZO!'... Hata Kama....”, ikionesha watoto wetu huko vijijini wakijisomea gazeti la Si Mchezo nyumbani kwao.

Akichangia, anonymous wa tarehe: 30/9/08 1:01 PM aligusia jambo moja muhimu, ambalo lilinikuna akili, pia:

“HIZI NYUMBA ZA NYASI ZITAKWISHA LINI VIJIJINI, JAMANI, na hawa watoto wetu nao wa(si)kulie katika mazingira yaleyale ya akina Zinjanthropus? No, this is not acceptable. Hata kama nyumba zote hazitaezekwa kwa bati, lakini angalau basi hata ujenzi wa kuta zenyewe za nyumba zionyeshe dalili ya uhai kidogo.
“Mazoea ni kitu kibaya. Wanasiasa wetu hodari sana kwa kuomba omba misaada. Wanangoja nini kuwaelimisha hao wanavijiji wetu angalau hata teknolojia asili ya kufyatua matofali na kuyachoma na kisha kujenga nyumba za kisasa kulingana na uwezo uliopo pale kijijini? Makazi Bora kwanza ndipo Kilimo cha Kisasa kisha Elimu Bora ikifuata Afya ya Kinga na hatimaye Viwanda na Maendeleo zaidi huko vijijini!
“Mjengwa, unasemaje kuhusu hilo? Huwa inanitia uchungu sana karibu nchi nzima kila uendako vijijini karibu asilimia 96% ya nyumba zote za makazi ya watu ni za nyasi tupu! Nyumba za Bati na Matofali ni za kubahatisha tu. Mafanikio ya wanasiasa wetu ni nini basi? Kutuwekea viwanda vinavyotengeneza bia nusu lita ikauzwe kwa shilingi 1,200/= au zaidi? Kupata maji safi na salama huko vijijini ni sawa na kuwa na mgodi wa dhahabu? Where are heading to?”
Wa-Tanzania wengi wameona hiyo picha niliyoweka hapo juu (Rais Bwana Jakaya Mrisho Kikwete akitoka katika nyumba moja ya m-Barbaig alipokitembelea Mkoa wa Manyara hivi majuzi).

Katika picha hii, msaidizi wa Rais anainua nyasi zisiingie katika nywele za Rais wetu au kumchoma kichwani au kumwingia machoni. Ni matumaini yangu kwamba kwa wakaaji wa nyumba hiyo bughudha ya nyasi hizo yaiwaletei “msongo na mavune”; ni kitu cha kawaida tu!

Uzuri wa picha hii au niseme ujumbe wake una maana kubwa. Hapa hatumwoni Rais wetu akiingia ndani ya nyumba hiyo! Wala hatumwoni Rais wetu akiwa ndani ya nyumba hiyo! Wala hatujui katumia muda gani akiwa ndani ya nyumba hiyo! Tunamwona Rais wetu akitoka nje kwa kuinama.

Si ajabu mgongo wa Rais wetu uliuma kwa kuinama! Si ajabu magoti ya Rais wetu yaliuma kwa kuinama! Si ajabu Rais wetu kasema kimoyomoyo, “Uongozi una taabu”! Si ajabu Rais wetu kasema kimoyomoyo, “Kamwe sitaingia nyumba ya namna hii tena”!

Hata tukisahau niyoandika hapo juu, ukweli utabakia pale pale kuwa Rais wetu kaguswa na hali halisi ya maisha ya wananchi wetu wanaoishi katika nyumba hiyo, hasa, na wale walalahoi wengine wenye maisha ya namna hiyo popote pale Tanzania, kwa ujumla! Rais wetu kayaonja maisha ya ki-lalahoi!

Mosi, Rais wetu hana budi kuutafsiri huo “msongo na mavune” yaliyomsibu kwa kuiangalia hiyo nyumba ya m-Tanzania wake kabla ya kukaribishwa au kujikaribisha ndani.

Pili, Rais wetu hana budi kuutafsiri huo “msongo na mavune” yaliyomsibu alikiingia ndani.

Tatu, Rais hana budi kuutafsiri huo “msongo na mavune” yaliyomsibu akiwa ndani amechuchumaa, amesimama ama amekaa!

Nne, Rais hana budi kuutafsiri huo “msongo na mavune” yaliyomsibu akitoka nje ya nyumba hiyo!

Kama kweli Rais wetu kaguswa na “msongo na mavune” hayo, ajue kuwa hiyo ni nyumba na maisha ya m-Tanzania (au wa-Tanzania) waliopiga kura katika uchaguzi uliopita. Si ajabu walikipigia Chama cha CCM na kumpigia mgombea wake Jakaya Mrisho Kikwete awe Rais wa Tanzania!

Rais wetu hana budi kuutafsiri huo “msongo na mavune” kutokana na ahadi yake kwa wa-Tanzania wa namna hiyo waliomsikia akiwika Bungeni (Desemba 30, 2005): “Maisha Bora kwa Wote”!

Kama kweli kaguswa na hali halisi ya maisha ya namna hiyo, angalau kwa dakika sijui ngapi alizotumia humo ndani ya nyumba hiyo, nachukua nafasi hii kumwomba Rais wetu aungane na wasomaji wengine, na wote warejee makala na hoja za dhati zinazojitokeza za mwandishi Joseph Mihangwa, Wabunge Wanapolilia Mkia wa Kondoo” (Toleo Na. 049) la Raia Mwema (au http://raiamwema.co.tz/).

Mengi yameandikwa hivi karibuni juu ya kero hii, kama Mbunge Wilbord Slaa (Karatu-Chadema) alivyolitaadhari taifa juu ya w a-Bunge kujiongezea mapesa! Na bila kusahau kuibiwa kwa u-wazi na makusudi kwa fedha za umma katika BoT na wale wote waliotoa siri kwa hao wezi kuwakaribisha na kufanikisha wizi huo!kuiba hizo,

Ningependa Rais wetu, Bwana Jakaya Mrisho Kikwete, na wa-Bunge wake, ikiwa ni pamoja na viongozi wa mihimili mingine muhimu ya serikali, waahidi na kutekeleza kwa vitendo kaulimbiu ya “NEVER AGAIN” ku- “acquiesce” na maisha duni ya namna hii! Yaani, tutoke nje ya mazingira ya namna hii, kama Rais wetu anavyotoka nje ya nyumba hiyo!

Lakini cha ajabu ni kwamba picha, kama hizi, huwa tunapenda kuziangalia tu na wakati mwingine kuziondoa upesi, upesi machoni mwetu (sisi wenye uhondo wa ulalaheri) bila kuzitafakari kwa nia ya kuleta maendeleo nchini kwa wale wenzetu ambao wanazidi kukandamizwa na ualalahoi.

Tusiimbe au tusilaani tu kaulimbiu za “Ari Mpya, Nguvu Mpya, Kasi Mpya”, “Maisha Bora kwa Wote” au “Maisha Bongo ni Tambarare”! Swali la changamoto kwa wote: Je, nyumba ya namna hiyo tunawezaje kuibadilisha iwe ya kisasa?

Hebu twende na mabadiliko ya nyumba hii, huku tukizingatia kwamba mabadiliko ya nyumba hii ni mabadiliko ya wakaaji wake, pia!

Naendeleza hoja yake: Nyumba hiyo iifanyiwe “make-over” ya kujengwa kwa matofali mabichi. Isiezekwe kwa bati, bali kwa nyasi ili kukinga joto na mvua. Ikiezekwa kwa bati, itakuwa tanuru wakati wa jua kali. Bila dari, wakati wa mvua ya mawe, itakuwa mlio wa bunduki; usiku hakuna kulala!

Tuanze kutumia akili zetu, polepole. Hayo ya “ari mpya, nguvu mpya, kasi mpya” yasiwe tu maneno ya ki-siasa: maneno matamu; ahadi tamu za kupata kura tuingie Ikulu, u-Bunge, u- Wakilishi wa Serikali za Mitaa au tupate kazi huku tukiwasahau wakulima, wavuvi. wachungaji, wawindaji mwiruni, waokotaji mwituni!

Tukiacha maisha yaende kwa ndoto zake za ki-“evolution”, itatuchukua pengine karne nyingi kuweza kubadilika kutoka nyumba ya kwanza kwenda nyumba ya pili, kama zinavyoonyeshwa hapo chini.

Lakini tunaweza, kwa akili zetu za leo, kabisa tukavuka hizo karne kwa kuingilia kati (to purposefully intervene) na kubadilisha nyumba, kama hiyo anayotoka Rais wetu Bwana Jakaya Mrisho Kikwete huko kwa wa-Barbaig.

Tutoke kabisa katika nyumba ya namna hiyo na tuingie, angalau, nyumba kama hizo za juu:

Nyumba hiyo izidi kufanyiwa “make-over”. Tunazo nyumba nyingi zilizofikia hali hii, ambazo hazina budi zifanyiwe “make-over”, pia, kwa kuweka milango, na madirisha hata ya vioo na mapazia, kama ilivyo mifano ya nyumba hizi zilizoko kwenye picha hapo juu ;

Tuzidi kupiga hatua kwenda mbele na kuweka umeme (uzalishwao na maji, mionzi ya jua au upepo) na gesi ya kupikia, endapo wenye gesi hawataiuza kwa nchi za nje hata kabla ya kukidhi mahitaji ya wa-Tanzania. Si gesi ni yao 75%; wanailipa Tanzania “royalties” na gesi itauzwa, kwa mfano, Kenya!

La sivyo, bila kuwaelekeza wa-Barbaig itawachukua tena karne kumi kuweza kubadilika, ama wasibadilike kabisa!

Kwa vyovyote vile, tunaweza tukafanya mapinduzi ya kutoka nyumba picha ya kwanza kwenda picha ya tatu bila kupitia kwa “mkunga-nyumba” (mid-wife) picha ya pili!

Lakini huenda mapinduzi ya namna hiyo yakawa ni makubwa sana kwa wa-Barbaing na walalahoi wetu wengine! Tutawafanya waathirike “na msongo na mavune” (stress and strain) au kwa lugha nyingine, “future shock” shauri ya kufika kwa “vya usasa” ambayo hatukujitayarisha kuvipokea (the sudden arrival of the future for which they are not prepared)!

Huku tukiandaa maisha yao yaende sambamba na mabadiliko ya nyumba zao, yatubidi twende na baadhi ya walalahoi wetu wengine pole pole, hasa wale wanaolegalega (the laggards) ili tufanikiwe kuwavusha.

Kwa kifupi, tunaweza kabisa kubadilisha maisha (utamaduni wa nyumba bora na mazingira) ya walalahoi wetu pole pole kwa kuanza na wale wapendao. Na baada ya miaka ishirini hivi, mazingira yetu huko vijijini yatabadilika kabisa na kuwa ya “usasa”! Hii haina budi kuwa sera ya maendeleo na wala si ya ki-siasa

Na kwa wa-Tanzania wengine wa vijijini, achaneni na nyumba za bati (kama hamna pesa za kununulia hayo bati). Jengeni na ezekeni kwa nyasi! Tumieni hizo pesa za mabati kununulia samani na mahitaji mengine ya lazima! Cha kujihadhari ni moto kwa nyumba zetu hizo zilizoezekwa kwa nyasi!

Angalieni mifano ya picha za nyumba tano za namna hiyo hapa juu:

Wakati akianza kazi ya u-Rais, Bwana Jakaya M. Kikwete aliahidi kuboresha ajira kwa vijana wetu kiasi cha milioni moja kila mwaka. Sawa. Lakini ahadi ni deni!

Tunaweza kabisa kukidhi na kuzidi kuwapatia ajira-manufaa (functional employment) kwa vijana wa Tanzania, huku wakishiriki katika mchakato wa kuboresha maisha ya walalahoi vijijini.

Sababu ya kutaka kutoa ajira-manufaa tunayo. Kinachokosekana ni uongozi (akili) wa ki-siasa. Na ahii inatokana kwa sababau viongozi wetu wengi wanashughulika kutengeneza “fweza” kutokana na michakato ya u-binafsi, kiasi cha kukosa nafasi au kutumia akili zao za uongozi kwa vya umma!

Kuna haja ya kujenga "brigedi" za vijana wasio na kazi, ki-mikoa, ki-wilaya na ki-tarafa: brigedi za kufyatua matofali (ikiwezekana ya kuchoma – sio lazima); kujenga nyumba; brigedi za useremala na utengenezaji wa samani za nyumbani; au brigedi za ushoni (ikiwa ni pamoja na magodoro ya kukalia na kulalia na mapazia na kufuma mazulia kwa katani na makuti na ukindu! Mapesa ya JK yamwagwe huko!

Huenda tukafanikiwa kubadilisha mitindo mazingira ya wana-vijijini (pamoja na maisha ya walalahoi wetu). Hii italeta nyumba bora vjijini pamoja na kuchangia maisha bora kwa wote. Miktadha ya hizo nyumba ni lazima iendane na mabadiliko ya akili, usafi wa mazingira, na vitu vya kutumia nyumbani.

Kuweza kuleta maisha bora kwa wa-Tanzania wetu ni lazima tupambane kuyaboresha kwa kutumia mbinu zote za vita hii. Vita yenyewe ni “frontal” –pande zote za mstakabali wa binadamu!









Barua pepe: romuinja@yahoo.com



Steers ndani ya Dar es Salaam wao wanakwambia "REAL FOOD MADE REAL GOOD". Haya mambo tena...






Utamu wa raha watu wa Mwambao!!!

Tuesday, June 16, 2009










Bendi Maarufu ya Mziki wa Dansi The Ngoma Africa inayoongozwa na mwanamziki Ras Makunja aka Bw.Kichwa Ngumu,imedatisha washabiki katika maonyesho ya kimataifa ya
Masala Festival,mjini Hannover,Ujerumani onyesho hilo liliofanyika jumapili ya 14-06-2009,
Bendi hiyo hilipanda jukwaani na kuanza kulishambulia jukwaa kwa mdundo mkali wa dansi la bongo ambalo dakika chache tu kulikuwa pata shika la asiye na mwana abebe jiwe! washabiki wote walikuwa wamedatishwa akili na mdundo huo.


Sunday, June 14, 2009











Leo bado niko Tanga kunani... pale kwenye soko la mjini(Uzunguni) ambapo mtazamo mzima uko kwenye kitoweo. Ingawa wakazi wengi wa mjini hapo upendelea sana kula samaki lakini nyama ya ngombe nayo ni mojawapo ya kitoweo kikubwa sana. Hili Bucha husifika kwa kuwa na nyama nzuri na freshi.