Friday, August 30, 2013

RAIS KIKWETE AMUOMBA RAIS WA UGANDA AONGEE NA KAGAME ILI KUMALIZA UGOMVI ULIPO

RAIS Jakaya Kikwete, amewasiliana na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, ili azungumze na Rais wa Rwanda, Paul Kagame kwa nia ya kumaliza mvutano wa maneno kati yao kwa busara.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alisema hayo jana bungeni, alipokuwa akijibu swali la Kiongozi wa Upinzani bungeni, Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe (Chadema).

“Tunataka suala hili limalizike kwa njia ya busara, ili watu waendelee kuchapa kazi, ninaamini busara zitatumika kumaliza tatizo hilo,” alisema.
Akiuliza swali katika kipindi cha maswali ya Papo kwa Hapo kwa Waziri Mkuu jana, Mbowe alitaka kujua kauli ya Serikali na mikakati iliyopo kupata suluhu katika mvutano wa maneno uliojitokeza kati ya Rais Kikwete na Rais Kagame.

Pia Mbowe alitaka Serikali kuunda jopo la ushawishi wa kimataifa, kutokana na Rwanda kuonekana kushawishi nchi za Uganda na Kenya, jambo ambalo linaashiria kuitenga Tanzania katika shughuli mbalimbali za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kwa mujibu wa Mbowe, kitendo cha marais wa Kenya, Uganda na Rwanda kukutana katika mikakati ya kuanza kutumia bandari ya Mombasa ambayo ingekuwa ya nchi za Afrika Mashariki, ni dalili kuwa Tanzania imeanza kutengwa.

Mbowe alisema pamoja na kuanza kutengwa kwa Tanzania katika shughuli za Afrika Mashariki pia kumekuwa na mgogoro uliozuka hivi karibuni wa Bunge la Afrika Mashariki, kutaka vikao vya Bunge hilo vifanyike kwa kupokezana katika nchi wanachama, tofauti na ilivyokuwa awali, ambapo vikao hivyo vilifanyika Arusha.

Hata hivyo, Pinda katika jibu lake, alisisitiza kuwa hakuna sababu ya Serikali kuunda jopo la kutafuta ushawishi wa suluhu na Rwanda kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), kwa kuwa hakuna sababu za kufanya hivyo.

Hakuna uhasama Akifafanua, Pinda alisema Serikali haina sababu ya kujenga uhasama na Rwanda, kwa kuwa nafasi ya Tanzania na mchango wake katika nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu na Afrika unajulikana.

Alisisitiza, kuwa ushauri aliotoa Rais Kikwete wa kutaka Rwanda kukaa meza moja na waasi, ulikuwa wa busara na haukuwa na tatizo lolote.

Kutokana na msingi huo, alifafanua kwamba ndiyo maana Tanzania haiangalii mvutano huo wa maneno kama tatizo, ingawa Serikali haitapuuza suala hilo linaloonesha kuwepo kwa dalili ya kutoelewana.

“Ukilitazama suala hili huwezi kuamini kama kweli kauli ya Rais Kikwete ingeleta haya, nadhani wenzetu wanalitazama kwa namna tofauti na sisi tunavyolitazama,” alisema.

Pinda alirejea kiini cha mtafaruku huo, kuwa ni ushauri wa Rais Kikwete kwa nchi ya Rwanda kukaa meza moja na waasi, ili kuacha mapigano kwa maslahi ya wananchi wa Rwanda.

Alisema kauli hiyo iliyotolewa na Rais Kikwete katika mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika Ethiopia, ilikuwa na nia njema kwa maslahi ya Rwanda, lakini imechukuliwa tofauti nje ya mkutano huo.


Propaganda za biashara
Katika hatua nyingine, Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk Charles Tizeba, alisema kauli zinazotolewa kuwa mizigo ya Rwanda haitapitishwa kwenye bandari ya Dar es Salaam, ni propaganda za kibiashara kutoka nchi washindani.

Hata hivyo, Dk Tizeba hakuwa tayari kubainisha ni nchi ipi inahusika zaidi kutoa propaganda hizo ingawa aligusia kwamba ni nchi zenye bandari.

Alisema baada ya kukutana na wafanyabiashara wa Rwanda na viongozi wa Serikali ya nchi hiyo, wamebaini kuwa hakuna upande uliozuia mizigo kupita Tanzania.

“Huku wanasema kuna maelekezo kwamba wafanyabiashara wa Rwanda wasipitishe mizigo Tanzania, lakini kwa Rwanda wao wanasema Tanzania imezuia mizigo ya Rwanda kupita Tanzania … tumebaini kuwa kauli hizi hazikuwa na ukweli,” alisema.

Alisema wafanyabiashara wa Rwanda wamesema kama Tanzania wanataka Rwanda ipitishe mizigo mingi, ifanye marekebisho kadhaa, ikiwemo kukabiliana na matatizo kama lililowahi kutokea la kupotea kwa kontena mbili za dhahabu na mbolea, kuangalia tozo za kusafirisha magari yasiyosajiliwa Tanzania na kupunguza wingi wa mizani ambao wanadai unachelewesha usafirishaji.

Pia Tizeba alisema walilalamikia udokozi wa vitu vidogo kwenye magari bandarini, jambo ambalo limefanyiwa kazi na hali hiyo haipo tena, kwani baadhi ya magari vifaa vyao vilikuwa vikiibwa maeneo mengine kabla ya kufika Dar es Salaam.

“Kuna mambo mengi yanafanyiwa kazi ikiwamo kuwa na treni mbili za mizigo hadi Isaka, ambazo zitasafirisha mizigo ya Rwanda, Kongo na Burundi, na pia kuweka ofisa wa bandari Kigali, ambaye atakuwa akishughulikia matatizo na kuanzisha mizani ambayo itapima gari likiwa linatembea na kuwa na mizani maeneo matatu,” alisema.

Kuhusu hatua ya Rais Kagame kuzindua mpango wa nchi yake kutumia bandari ya Mombasa, Tizeba alisema nchi inaweza kuwa na njia nyingi za kupitishia mizigo, na kubainisha kuwa bado Tanzania ndilo eneo pekee zuri kwa kusafirisha mizigo kwa nchi zisizo na bandari.

REDD'S MISS TANZANIA BRIGITTE ALFRED AAGWA RASMI JIJINI DAR.

Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mh. Dkt. Fenella Mukangara (wa pili kulia) akitoa nasaha zake kwa Warembo wanaowania taji la Redd's Miss Tanzania 2013,wakati wa hafla ya Chakula cha jioni ikiwa ni sehemu ya kumuaga Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigitte Alfred.
Hafla hiyo imefanyika usiku huu kwenye Hoteli ya Giraffe,Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni kutoka wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Herman…
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Lino International Agency ambao ni Waandaaji wa Shindano la Miss Tanzania,Hashim Lundenga akimuaga Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigitte Alfred (katikati) mara baada ya kukabidhiwa Bendera ya Taifa na Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mh. Dkt. Fenella Mukangara (kulia) wakati wa hafla ya Chakula cha jioni kwa ajili ya kumuaga Mrembo huyo,iliyofanyika kwenye Hoteli ya Giraffe,Jijini Dar es Salaam usiku huu.

DIAMOND NOMA:AMZAWADIA MZEE GURUMO GARI MPYA KATIKA UZINDUZI WA VIDEO YAKE MPYA "NUMBER ONE"


AKIMKABIDHI MZEE GURUMO KARI 

Diamond Platnumz jana alifanya uzinduzi wa video ya wimbo wake mpya, Number 1 kwenye ukumbi wa Serena Hotel jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huo ulihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo ndugu zake, marafiki, wasanii wenzake na wadau mbalimbali wa muziki nchini.

Kwenye uzinduzi huo pia, Diamond alimpa zawadi ya gari msanii mkongwe aliyetangaza kustaafu muziki, Muhidin Gurumo kama heshima kwake.

KANALI FEKI WA JESHI ANASWA SHUGHULI PEVU YAFANYWA KUMKAMATA

Na Issa Mnally
IBRAHIM Moses, mkazi wa Mwenge jijini Dar es Salaam amenaswa na Polisi wa Kituo cha Mwenge kwa madai ya kujifanya askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) mwenye cheo cha kanali.
Kanali feki wa JWTZ, Ibrahim Moses baada ya kunaswa na polisi.
Kijana huyo alinaswa na polisi kwa kushirikiana na maafisa wa JWTZ baada ya kuwekewa mtego kutokana na kudaiwa kuwa alikuwa anajiita Kanali Ibra, hivyo kutiliwa mashaka hasa baada ya siku moja kuonekana akiwa na pingu.
Habari za kipolisi zinadai kuwa Ibra alikuwa akifika Kituo cha Polisi Mwenge mara kwa mara na alikuwa akipewa heshima zote kama afisa wa jeshi na hasa kwa kuwa alikuwa akitoa ushirikiano wakati wa kunasa wahalifu.
...Akiwa mikononi mwa polisi.
“Alikuwa akija kituoni na kujifanya ni Kanali Ibrahimu akiwa na gari lake, hivyo kupaki na kupatiwa ulinzi mpaka shughuli zake zinapokwisha maeneo hayo.
“Ilikuwa akikuta watu wamejazana hapa kituoni alikuwa anakuwa mkali na kuhimiza washughulikiwe haraka kwani hapendi kuona watu wamejaa kwenye kituo,” kilisema chanzo chetu kituoni hapo.
...Akipelekwa kituoni.
Chanzo hicho kilidai kuwa walianza kumtilia mashaka baada ya siku moja kumuachia mfuko wake askari mmoja ambaye alipoudadisi alikuta kuna pingu, hivyo polisi kuulizana inakuwaje kanali wa jeshi atembee na pingu.
Habari zinasema baada ya hapo mkuu wa kituo hicho cha polisi ilibidi afanye kazi ya ziada kuwasiliana na wanajeshi wa Kambi ya Lugalo ili kujua kama wana afisa wao anayeitwa Kanali Ibrahimu Moses wa Kitengo cha Usalama wa Taifa na Mawasiliano, wakajibu hawakuwa na askari mwenye jina hilo ndipo ulipoandaliwa mtego wa kumnasa.
Imeelezwa kuwa aliitwa kituoni hapo kwa njia ya simu na kuambiwa kulikuwa na kazi ya kiintelejensia na baada ya saa tatu akawa amewasili na kukamatwa kisha kufungwa pingu na kupelekwa Kituo cha Polisi Kijitonyama, Dar kwa mahojiano zaidi ambapo afisa mmoja amesema atafikishwa mahakamani wakati wowote.
Source:global publishers

SHEIK PONDA AFIKISHWA MAHAKAMANI TENA.....KESI YAAAHIRISHWA HADI SEPTEMBA 11


Kiongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda jana alisababisha kusimama kwa shughuli za Serikali wilayani Morogoro baada ya ofisi kadhaa ikiwamo ya Mkuu wa Wilaya na baadhi ya mitaa kufungwa ili kupisha kusikilizwa kwa kesi inayomkabili katika Mahakama ya Mkoa wa Morogoro. 
  
Tofauti na Agosti 19, mwaka huu wakati aliposafirishwa kwa helikopta, jana Sheikh Ponda alisafirishwa kwa barabara kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro akiwa chini ya ulinzi.
 
Mbali ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Morogoro kufungwa, nyingine ni Hazina Ndogo, Madini, Posta, Vipimo, Ukaguzi na Maktaba ya Mkoa.
 
 
Sababu za kufungwa kwa ofisi hizo pamoja na Mtaa wa Stesheni na maeneo ya Posta ni kuwa jirani na Mahakama hiyo. Magari yalizuiwa kutembea katika njia na maeneo ya karibu na ofisi pamoja na Mahakama hiyo huku kukiwa na idadi kubwa ya askari polisi na magereza kwa muda wote wa takriban saa mbili.
 
 
Alifikishwa mahakamani hapo saa 4:10 asubuhi akiwa katika basi la Magereza ambalo lilisindikizwa na jingine dogo, huku magari mengine yakisimamishwa kupisha msafara huo. 

Mahakama hiyo ilifurika umati wa wafuasi wa kiongozi kiasi cha kuwalazimu polisi na wana usalama wengine kuweka utepe kuwazuia wengi wao kufika katika jengo lililokuwa likitumika kuendesha kesi hiyo.
 
 
Shughuli katika eneo hilo zilirejea katika hali yake ya kawaida saa 6:25 mchana baada kesi yake kuahirishwa na msafara wa Sheikh Ponda kurejea katika Gereza la Segerea, Dar es Salaam ambako yuko rumande.
 
 
Muda wote tangu kuwasili mpaka kusikilizwa kwa kesi hiyo, wafuasi hao walikuwa kimya hadi pale ilipoahirishwa na hasa baada ya Sheikh Ponda kuwapungia mkono alipokuwa akielekea kwenye basi ambako walisikika wakisema: 

“Takbriir na kuitikia Allahu Akbar – (Mungu Mkubwa).”
 

Kesi yenyewe
 
Katika kesi hiyo, Wakili wa Serikali, Benard Kongola alisema mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Morogoro, Richard Kabate kuwa Sheikh Ponda alitenda makosa ya uchochezi Agosti 10, mwaka huu saa 11.45 jioni kwenye maeneo ya Kiwanja cha Ndege, Morogoro.
 
 
Alisema siku hiyo, Sheikh Ponda alialikwa kutoa maelezo machache kwenye Kongamano la Eid lililoandaliwa na Umoja wa Wahadhiri Mkoa wa Morogoro (Uwamo) na kwamba akiwa hapo alitamka maneno: 

“Ndugu Waislamu, msikubali uundwaji wa kamati za ulinzi na usalama za misikiti kwani kamati hizo zimeundwa na Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata), ambao ni vibaraka wa CCM na Serikali na kama watajitokeza kwenu watu hao na kujitambulisha kwamba wao ni kamati za ulinzi na usalama za misikiti, fungeni milango na madirisha ya misikiti yenu na muwapige sana,” huku akijua kutoa maneno hayo ni kosa kisheria.
 
 
Alisema kwa kufanya hivyo, Sheikh Ponda anayetetewa na mawakili watatu wanaoongozwa na Juma Nassoro, alivunja masharti ya Mahakama ya kifungo cha nje iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya Mei 9, mwaka huu iliyokuwa imetamka kuhubiri amani.
 
 
Katika shtaka la pili, Sheikh Ponda anadaiwa kuwashawishi wafuasi wake kutenda kosa la jinai kwa kuwaambia: 

Serikali ilipeleka jeshi Mtwara kushughulikia suala la vurugu iliyotokana na gesi kwa kuwaua, kuwabaka na kuwatesa wananchi kwa sababu asilimia 90 ya wakazi wake ni Waislamu, lakini haikufanya hivyo kwa wananchi wa Loliondo waliokataa Mwarabu asipatiwe kipande cha ardhi ya uwindaji baada ya kudai ni mali yao kwa sababu asilimia 90 ya wakazi wake ni Wakristo.” 


Shtaka la tatu ni kudaiwa kutamka maneno yaliyoumiza imani ya watu wengine kama yalivyo katika shtaka la pili.

Baada ya kusoma mashtaka hayo, Kongola alisema walikuwa na mashahidi 15 na vielelezo vitatu ambavyo ni DVD mbili na kibali kilichotolewa na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Morogoro(OCD), Agosti Mosi, 2013 cha kongamano husika na hati ya hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Kisutu, Mei 9, 2013.
 
Baada ya kusomewa, Sheikh Ponda alikana mashtaka yote matatu huku akikubali kuwemo kwenye kongamano hilo. Alikiri kukamatwa na polisi Agosti 11, Dar es Salaam.
 
Wakili wa utetezi, Nassor aliwasilisha ombi la dhamana kwa mteja akisema mashtaka hayo yote kisheria yana dhamana. 
  
 Pia aliwasilisha ombi la kupatiwa hati yenye maelezo ya mlalamikaji ambaye ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwani alisema kuwa kutokana na upelelezi upande wa mashtaka kukamilika, wanahitaji maelezo hayo kwa ajili ya kuandaa utetezi.
 
Hata hivyo, Wakili Kongola aliiomba Mahakama kutompa dhamana mshtakiwa kutokana na cheti kilichotolewa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), kupinga dhamana ya mshtakiwa huyo kwa masilahi ya usalama wa nchi.
 
Akitoa mwongozo wa maombi yaliyowasilishwa na pande zote mbili, Hakimu Kabate aliahirisha kesi hiyo hadi Septemba 11, mwaka huu itakapotajwa tena na kwamba Septemba 17, mwaka huu Mahakama itatoa uamuzi endapo mshtakiwa atapewa dhamana au la wakati itakapoanza kusikilizwa.

CHUPI NA SHANGA ZA MSANII SHILOLE ZAANIKWA NJE- FIESTA


Monday, August 26, 2013

WATOTO WA KIKE, TUWAFICHE WAPI WASIYAONE MAPENZI?


Mwanzoni mwa juma hili,nilitembelea shule moja ya wasichana nikiwa na shida ndogo ya kiofisi hapo.
Jina la shule naomba nilihifadhi sina taaluma ya uandishi wa habari,nisikiuke misingi yake.
...
Nilipofika ofisini nilikaribishwa staff ya walimu,nikaambiwa nisubiri.Hapo ndipo niliduwaa kumuona mwalimu mmoja wa kike akiingia ofisini na mtoto wa kike,kidato cha tatu huku akiandamwa na fimbo za mgongoni.
...
Tatizo lilikuwa kwamba,,yule binti alikuwa amekamatwa jumapili yake(siku iyo ilikuwa jumatatu)
Akiwa amelala na wanaume wawili wakati wenzake wameruhusiwa kwenda nyumba ya ibaada.Shule yenyewe ina taratibu ya kuwaruhusu wanafunzi kuhudhuria ibaada nje ya shule ambapo ni mwendo wa dk 25 ivi kwa miguu... Mwanafunzi huyu alikiri kulala na wanaume hao wawili na alipoulizwa aliwafaham vipi,alisema alitumia simu ambayo pamoja na shule kuzuia bado aliiweka kwenye taiti,,ikiwa na vibration.Aliweka wazi kuwa matroni hata akague vipi hawezi kuwakamata wote maana wanafunzi wengi wana simu.
...
Alipoulizwa anapaje ujasiri wa kulala na wanaume wawili,huku akilia anasema alikubaliana na mmoja,akaongezeka wa pili,,hivyo asingeweza kuwazuia.
...
Tukio hili ambalo bado linaendelea kuchukuliwa hatua stahiki ikiwemo wahusika kutafutwa,,lilinifanya niondoke na maswali mengi kichwani.Je tuwafiche wapi? Je malezi gani tuyatumie? Je wazazi walio nyumbani wanajua watoto wao wanamiliki simu? Je imefika mahali,somo la Mahusiano Urafiki Mawasiliano na Mapenzi liwekwe shuleni? Je hawa ndo wake wema na waume wema wa kesho?
Iliniuma,,jamani tusitafute wa kulaumu bali nini kinaweza kuleta usalama.

MCHAWI AANGUKA AKIWA KWENYE HARAKATI ZA KULOGA

Mchawi hivi karibuni kaleta kizaa zaa huko Dzivarasekwa alipokutwa na 'birthday suit' yake(uchi)

Sabina Rokuzhe alikiri kuwa yeye ni mchawi na amedondoka alipokuwa anaruka kwenye ungo akitokea kwenye trip yake ya kuloga huko Masvingo.


Alikutwa kwenye nyumba ya Mbuya Annah Kamupaundi. AkaaAnza kuwaomba watu waliomzunguka wasimpige ,akasema pia katembelea nyumba kadhaa katika eneo hilo.


Mmoja wao aliyemuona asubuhi mapema ni Mrs Alice Hundi (37) ambae alisema aliamka baada ya kusikia mayowe ya mwanamke kwenye saa nane hivi usiku.


"Nilipomuona yuko uchi,nilimmwagia chumvi usoni, akaanguka na kuanza kujizungusha zungusha chini. Tuliita polisi na akachukuliwa"

KANISA LACHOMWA MOTO JIJINI DAR

Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Jimbo la Kati, Usharika wa Segerea Wilaya ya Ilala, limechomwa moto na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jana. 


Tukio hilo lilitokea saa saba usiku, wakati waumini wa kanisa hilo wakiwa katika mkesha wa maombi ya maandalizi ya mkutano wa injili unaoanza leo.


Mchungaji wa kanisa hilo, Noah Kipingu alisema wakati wakiwa katika maombi ghafla walisikia sauti ya kitu kilichorushwa kutoka nje ya kanisa kikiambatana na moto, ambapo kilianguka madhabahuni na kuanza kuunguza baadhi ya vifaa vya kanisa.


“Tukiwa tumesimama mbele ya madhabahu kwa njia ya mduara ndipo nyuma ya madhabahu ukatokea mlipuko mkubwa kwa sauti ya kishindo, na moto ukatanda madhabahu,” alisema Kipingu na kuongeza kuwa:


“Katika namna ya kibinadamu hakuna aliyeweza kuvumilia, kila mtu alikimbia akitafuta namna ya kujiokoa.”


Kipingu alisema kuwa alipobaini kuwa ulikuwa ni moto wa mafuta aliwaambia waumini wake waingie ndani kwa ajili ya kuuzima, wakati wakiuzima moto huo walipata taarifa kuwa gari la Mchungaji, Toyota Cresta lenye namba za usajili T 482BAF lililokuwa nje ya kanisa lilikuwa likiwaka moto. 

“Baadhi ya waumini waliokuwa ndani walikwenda nje kushirikiana na mlinzi kuuzima moto huo, tunamshukuru Mungu kwamba matukio yote mawili tumeyashinda kwa uwezo wake,” alisema.


Kipingu alisema kuwa shambulizi hilo lilizua taharuki kubwa kwa waumini wake, na kwamba baadhi ya watu waliwaona watu wanne wakikimbia kutoka eneo la kanisa baada ya kutukio hilo.


Shukuru Thobias mmoja wa waumini waliokuwepo kanisani wakati tukio hilo likitokea, anasema aliona vitu kama mshale vikianguka madhabahuni na vilipodondoka vililipuka kama moto.


“Moto ulianza kuunguza Biblia na makapeti, ndipo tukaanza kukimbia kwenda nje kuchukua mchanga na kuanza kuuzima. 

"Baada ya hapo tulianza kukimbia huku wengine wakidondoka na kujeruhiwa kidogo miguuni. Niliporudi baadaye niligundua zilikuwa ni chupa tatu za bia zilizokuwa zimetengenezwa bomu la petroli,” alisema Thobias.


Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo hakuna mtu aliyepoteza maisha na kulitaja kuwa ni jaribio la kiharifu lililoshindwa.


“Hakuna mtu aliyepoteza maisha, lilikuwa jaribio ambalo halikufanikiwa. Wakati tukio linatokea waumini walikuwa kanisani kwa hiyo waliwahi kuuzima moto kabla haujaleta madhara,” alisema Kova.



Matukio ya makanisa kuchomwa moto
Mei 26, 2012, Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) lililopo Mtaa wa Kariakoo mjini Unguja, lilichomwa moto usiku na watu wasiofahamika.

WEMA SEPETU ADAIWA KUJIHUSISHA NA BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYA

Skendo ya mastaa mbalimbali Bongo kutajwa katika biashara na usafirishaji wa madawa ya kulevya ‘unga’ linazidi kuchukua sura mpya ambapo tayari majina ya wasanii wawili wakubwa, Wema Isaac Sepetu na Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’ yametajwa huku kinachowaponza kikijulikana.

Habari zinadai kuwa mastaa hao wameanza kujutia tambo zao za kutangaza utajiri walionao hivyo kuibua maswali kuwa huenda wana uhusiano na wafanyabiashara wa dawa za kulevya ikiaminika ndiyo njia ya haraka ya utajiri.

WEMA
Inadaiwa kuwa kitendo cha Wema kutangaza kununua nyumba, magari ya kifahari na kutapanya fedha ndiko kulikomponza na sasa anatajwa na wengi vinywani mwao juu ya kuhusika katika biashara hiyo haramu.

Kuna madai kuwa bosi huyo wa Endless Fame Productions amehojiwa juu ya suala hilo lakini meneja wake, Martin Kadinda alikanusha uvumi huo.

DIAMOND
Wiki iliyopita, Diamond aligeuka gumzo baada ya kuripotiwa akihusishwa na biashara hiyo huku ikidaiwa kuwa kinachomponza ni utajiri alioupata ghafla.

Ilidaiwa kuwa kitendo cha kutangaza kununua nyumba takriban tano jijini Dar, kumiliki kiasi cha Sh. bilioni moja kwenye akaunti na kuendesha magari ya kifahari ndivyo vilivyochangia watu kugeuzia antena za runinga zao kwake kutaka kujua ni matunda ya muziki tu au kuna kingine.

Madai ya jina la Diamond kutajwa katika saga hilo yalikwenda mbele zaidi ikielezwa kuwa kitendo cha kusafiri mara nyingi nje ya nchi huku akipiga picha na watu wanaosemekana kujihusisha na biashara hiyo nacho kilimponza.

Kwa upande wake, Diamond alisema kuwa hakuna mtu asiyejua namna anavyotafuta fedha kwa jasho juani hivyo watu wakimuona akila kivulini lazima wakumbuke kuwa amechumia juani na hajui chochote juu ya dawa hizo.

Tuesday, August 20, 2013

Mwanamke ajilipua kwa petroli baada ya mumuwe kuoa mke wa pili huko Geita.

MWANAMKE mmoja ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Nyankumbu, Kata ya Kalangalala mkoani Geita amenusurika kifo baada ya kujimwagia mwilini mafuta ya petroli kisha kujilipua baada ya mumewe kuoa mke wa pili. 

Imeelezwa kuwa mwanamke huyo, Anastazia Kubezya (28) Agosti 8 mwaka huu aliamua kujimiminia petroli mwili mzima kabla ya kuchukua kiberiti na kujilipua, hali iliyosababisha akimbizwe katika Hospitali ya Geita alikolazwa katika wodi namba saba kwa matibabu.

Akizungumza na mwandishi wetu, Consolata Raphael ambaye ni dada wa majeruhi huyo alidai kuwa chanzo cha mdogo wake huyo kufikia hatua ya kutaka kutumia njia hiyo ya mkato kwa lengo la kujiua ni wivu wa mapenzi.

Consolata alisema: “Siku ya tukio shemeji yangu George Kubezya (mume wa majeruhi), alifika nyumbani kwa mdogo wangu wa kiume akidai kuwa mkewe huyo anatishia kujiua baada ya kuoa mke wa pili.

“Tukiwa tunaendelea kujadiliana mara alitokea mkewe Kubezya akiwa na viatu vya mwanaye mdogo akamkabidhi mdogo wetu mwingine aitwaye Rozalia akamwambia mpatie mwanaye kwa kuwa anaondoka na hajui atarudi lini.

“Baada ya kutamka maneno hayo aliondoka na niliwasiliana na ndugu yetu mwingine aitwaye Elizabeth aliyesema Anastanzia alipita kwake akiwa na chupa ikiwa na petroli na walipojaribu kumkimbiza alipotelea gizani.


“Kati ya saa 4 na saa 5 usiku Eliza na wenzake walisikia mtu akilia nje ya nyuma yao na baada ya kutoka nje walikuta Anastanzia akiwa tayari amekwisha jilipua moto, walipomhoji alidai amefanya hivyo ili afe kutokana na mumewe kumuolea mke mwenza na kumleta kwenye nyumba waliyoijenga yeye na mumewe,”alisema Consolata. 

Hata hivyo juhudi za kumpata mumewe kuzungumzia sakata hilo hazikuzaa matunda baada ya kile kilichoelezwa kuwa alitoroka muda mfupi baada ya kumfikisha mkewe hospitalini.

Mwandishi wetu alifika hospitalini hapo na kukuta mwanamke huyo aliyelazwa wodi namba nane akiwa anauguzwa chini ya ulinzi wa polisi ili akipona afikishwe mahakamani kwa kosa la kujaribu kujiua.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Geita, Dk. Adam Sijaona akizungumzia hali ya majeruhi huyo alisema bado si nzuri na wanafanya mpango wa kumhamishia katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando iliyopo jijini M
wanza.

Ujumbe muhimu kwa wanaouza makalio yao mitandaoni.....


Unapiga Picha unaandika maneno mazuri tu na kupost Facebook ama Instragram ,''Asante Mungu kwa siku hii ya Jumatatu,AMEN''...


Cha kushangaza ni kwamba picha yenyewe umepiga makalio yako na umeyageuzia kwa watazamaji.Kwani kuna uhusiano gani wa Makalio yako na siku ya Jumatatu???

Au unamaanisha yana shape ya Jumatatu?Halafu wengine basi tu mnapenda kuweka lakini wala shape zenyewe sio kiivyo,sio kwa sababu yule kaweka basi na wewe unatuwekea mkusanyiko wako wa viazi vitamu na kaukau,unajishushia heshima....

Sio kila kitu ni cha kuiga,Huo ni ushamba na hamjui tu tunawatafsirije huku mtaani...

Serikali yakanusha kuwa Mama Salma Kikwete si Mnyarwanda na wala Kikwete si shemeji yao

Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO Assah Mwambene leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara hiyo amekanusha taarifa zilizoandikwa kwenye mtandao wa wa News for Rwanda na wanyarwanda kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ni shemeji wa aliyekuwa Rais wa Rwanda Juvenal Havyarimana. 

“Taarifa hizi haina ukweli wowote na zinalenga kumpaka matope Rais Jakaya Mrisho Kikwete,”amesema Mwambene na kufafanua kuwa lengo la mitandao ya kijamii ni kuhabarisha na kuelimisha umma wala siyo kupotosha jamii kwa kuandika habari zisizo na ukweli wowote.

Madai hayo yaliandikwa jana na mitandao ya Rwanda wakidai kuwa mama Salma Kikwete ni Mnyarwanda na ni binamu wa aliyekuwa rais wa zamani wa Rwanda. 

Monday, August 19, 2013

"WALIOPANDA MBEGU DECI WATARUDISHIWA"...MAHAKAMA

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imewahukumu kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya sh milioni 21 vigogo wanne wa iliyokuwa Kampuni ya Development Entrepreneurship for Community Initiative (DECI ).
Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Alocye Katemana, pamoja na adhabu hiyo pia ameiagiza serikali ifanye mchanganuo wa mali za DECI ambazo inazishikilia, kwa kuwa zipo mali zilishikiliwa zisizo za kampuni hiyo bali za watu wengine.

Alisema kuwa fedha za wateja wa DECI walizopanda zirejeshwe kwa wateja wenyewe ambao wataonesha uthibitisho wa kweli kuwa walipanda fedha zao huko.

Katika hukumu hiyo iliyotolewa na Hakimu Mkazi, Stewart Sanga na kusomwa na Hakimu Katemana, washitakiwa walikuwa watano, ambao ni Jackson Mtares, Dominick Kigendi, Timotheo ole Loitginye, Samwel Mtares na Arbogast Kipilimba.

Washitakiwa hao walikuwa wanatetewa na mawakili wa kujitegemea Hudson Ndusyepo na Onesmo Kyauke.

Hakimu Katemana alisema washtakiwa hao ambao ni wachungaji wa makanisa ya Pentekoste wametiwa hatiani kuanzia wa kwanza hadi wa nne, isipokuwa mshtakiwa wa tano ndiye ameachiliwa huru baada ya mahakama kumuona hana hatia katika makosa hayo mawili.

“Mahakama imeridhika kuwa upande wa Jamhuri uliokuwa unawakilishwa na Wakili wa Serikali, Prosper Mwangamila na Justus Mulokozi, umeweza kuthibitisha kesi yao na kwa maana hiyo mahakama inawatia hatiani washitakiwa hao wannne na kumwachilia huru mshitakiwa mmoja, kwa sababu mashitaka dhidi yake Jamhuri imeshindwa kuyathibitisha,” alisema.

Alisema katika kosa la kwanza kila mshitakiwa atapaswa alipe faini ya sh milioni tatu au kwenda jela miaka mitatu, na katika kosa la pili kila mshitakiwa atatakiwa alipe faini ya sh milioni 18 au kwenda jela miaka mitatu na kwamba mshitakiwa atakayeweza kulipa faini ataachiliwa huru.

Kabla ya hukumu, Hakimu Katemana, aliwapatia nafasi mawakili wa pande zote mbili kuzungumza chochote, ambapo Wakili wa Serikali, Mwangamila, alieleza kuwa washitakiwa ni wakosaji wa mara ya kwanza na kwamba makosa waliyoyatenda yana madhara katika uchumi wa nchi, hivyo akaomba wapewe adhabu kali.

Wakili wa washitakiwa, Ndusyepo, alidai kuwa wateja wake ni mara yao ya kwanza kutenda makosa hayo ambayo waliyatenda wakati wakiwa katika harakati za kuwakwamua waumini wao katika lindi la umaskini.

Aliomba mahakama isiwapatie adhabu kali kwani wateja wake hawana uwezo wa kulipa fidia, ikizingatiwa kuwa wengine ni wastaafu na hawana huwezo wa kifedha.

Jana saa 7:00 mchana, Wakili Ndusyepo aliliambia gazeti hili kuwa tayari ndugu wa Domick na Mtares walikuwa wakielekea benki na ofisa wa mahakama kwenda kulipa faini ili waweze kukwepa adhabu ya kwenda jela.

Juni 12 mwaka 2009, washitakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza, baada ya vuta nikuvute kati ya viongozi na wanachama wa DECI .

Wakili Mwangamila alidai washitakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka mawili ambayo ni kuendesha na kusimamia mradi wa upatu kinyume cha kifungu 111A (1,3) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16.

Alidai kuwa, kati ya mwaka 2007 na Machi 2009, katika makao makuu ya DECI , yaliyopo Mabibo Mwisho, jijini Dar es Salaam, washitakiwa waliendesha na kusimamia mradi wa upatu katika sehemu tofauti nchini, kwa ahadi ya kuwapa wanachama wao fedha zaidi ambazo katika mazingira ya kibiashara ni kubwa kuliko mradi waliokuwa wakiufanya.

Mwangamila alidai kuwa, shitaka la pili ni kupokea amana za umma bila kuwa na leseni, kinyume cha kifungu cha 6 (1,2) cha Sheria ya mabenki na Taasisi za Fedha Na. 5 ya mwaka 2006 na kwamba, washitakiwa wote katika kipindi hicho wakiwa kwenye ofisi zao za DECI , walipokea amana kutoka kwa umma bila leseni.

-Tanzania daima

Picha na habari kamili kuhusu vurugu zilizotokea jijini mwanza leo

MAANDAMANO ya amani yaliyokuwa yameandaliwa na chama cha demokrasia na maendeleo(chadema) yamegeuka shubiri kwa wakazi wa jiji la Mwanza baada ya kuibuka mapambano makali baina ya waandamanaji hao na jeshi la polisi mkoani Mwanza na kusababisha polisi kutumia nguvu kuwatawanya wafuasi wa chama hicho.


Maandamano hayo ya amani ambayo yalianzia katika eneo la Buzuruga nje kidogo ya jiji la Mwanza yalikuwa yakiongozwa na wabunge Highness Kiwia wa Ilemela pamoja na Ezekiel Wenje kuelekea katika viwanja vya Furahisha na yalilenga kumshinikiza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Ernest Ndikilo kutoa barua zinazodaiwa kuandikwa na ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi kuwarejesha madiwani watatu waliotimuliwa katika Manispaa ya Ilemela kutokana na kushindwa kuhudhuria vikao vitatu mfululizo.


Polisi wenye silaha pamoja na askari kanzu walianza kutanda katika eneo hilo la Furahisha wakiongozwa na Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai Mkoa wa Mwanza RCO Konyo ambaye alikuwa akitumia gari lenye namba za usajili DK 068EXV aina ya Toyota Land Cruiser


Maandamano hayo ambayo awali yalionekana kana kwamba yangelimalizika salama yaliwasili katika viwanja vya Furahisha majira ya saa 5.38 huku yakiongozwa na gari la polisi lenye namba za usajili za nchi ya Uganda 779 UAG likiwa nimesheheni polisi wenye silaha nzito ikiwa ni pamoja na mabomu ya machozi na bunduki pamoja na askari kadhaa ambao walikuwa katikati ya maandamano hayo.


Baada ya maandamano hayo kuwasili katika viwanja vya Furahisha kwa amani,waandamani hao ambao walikuwa na mabango mbalimbali yaliyosomeka kuwa :‘Matata hatutaki uendelee kuwa Meya wa Ilemela rudia kazi yako ya awali,.... na jingine Jaji Sumari tumechoka kuahirisha mara kwa mara kesi dhidi ya Matata ....na jingine lililosomeka kuwa RD Ndikilo tunahitaji barua za kurejeshwa kwa madiwani wetu.


Hata hivyo tofauti na ilivyokuwa imetangazwa kuwa maandamano hayo ya amani yangelipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Ernest Ndikilo,hakukuwa na kiongozi yoyote wa Serikali ambaye alikuwepo uwanjani hapo kupokea maandamano hayo.


Kufuatia kutoonekana kwa kiongozi yoyote wa Serikali,viongozi wa chadema pamoja na wabunge wao walikutana kwa faragha kwa dakika kadhaa kwa ajili ya kujua hatima ya maandamano hayo ambapo Mbunge wa Nyamagana Ezekiel Wenje alipanda jukwaani saa 6.45 na kuwaeleza maelfu ya waandamanaji kuwa wameamua kumtuma Mbunge wa Ilemela Highnes Kiwia kwenda ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kuchukua majibu kwa ajili ya kuwaletea wananchi walioandamana juu ya hatima ya madiwani hao.


Hata hivyo saa moja baadae Mbunge huyo alisimama jukwani na wakuwaeleza waandamani hao kuwa simu ya Mbunge Kiwia ilikuwa haipatikani hivyo kuwataka kuandamana kwenda kwa Mkuu wa mkoa wa Mwanza kujua kulikoni na hapo ndipo hali ya hewa ilipochafuka.


Jeshi la polisi baada ya kuona wandamanaji hao wameanza kuelekea katika ofisi za Mkuu wa mkoa liliwataka kutawanyika ambapo waandamanaji hao walikaidi ndipo jeshi la polisi lilipoamua kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi hao.


Vurugu hizo ambazo zilianza majira ya saa 7.30 zilisababisha kufungwa kwa baadhi ya barabara kutokana na waandamanji hao kuweka vizuizi vya mawe na kuchoma matairi,ambapo pia maduka na ofisi mbalimbali zililazimika kufungwa kwa muda kupisha vurugu hizo.


Baadhi ya wananchi ambao walikuwa wakitumia usafiri wa umma walionekana wakishuka kupitia katika madirisha ya magari hayo na kukimbia kwa hofu ya kujeruhiwa na mabomu pamoja na mawe ambayo yalikuwa yakirushwa na waandamanji hao kwa jeshi la polisi.


MKUU WA MKOA WA MWANZA ALONGA.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza akizungumza na Mbunge Kiwia pamoja na viongozi wa chadema ofisini kwake alisema kuwa ameshangazwa na uvumi huo kuwa ofisi yake imekalia barua za kurejeshwa kwa madiwani Abubakar Kapera(Nyamanoro),Dan Kahungu(Kirumba) pamoja na Marietha Chenyenge(Ilemela).


RC Ndikilo alisema kuwa Serikali imekuwa ikifanya kazi zake kwa maandishi na sio kwa kufuata maneno ya mtaani na kueleza kuwa hana barua yoyote toka ofisi ya Waziri Mkuu inayomualifu kuhusu kuwarejesha madiwani hao baada ya kukata rufaa.


“We Mbunge kuna siku ulinipigia simu ukiniuliza juu ya kuwepo kwa barua hizo nami nilikujibu kuwa kwa kuwa uko hapo Bungeni Dodoma ambapo pia kuna ofisi ya Waziri Mkuu nilikujibu kuwa ni muhimu ukawaona viongozi wakuu wa Tamisemi ikiwa ni pamoja na Waziri Mkuu,pia nilikushauri kuwa wakupe japo nakala ya barua hiyo”,alisema RC Ndikilo.


“Lakini cha kushangaza nimekuwa nikisikia maneno ya ajabu kuwa nimeficha barua za madiwani hao,ikumbukwe kuwa madiwnai hao hawakukata rufaa kwangu bali walikata rufaa ngazi ya juu kabisa,ili kukata mzizi wa fitina naomba kati ya tarehe 26 hadi 27 wewe Mbunge pamoja na mimi twende TAMISEMI kukutana na viongozi ili kukata mzizi wa fitina na tuje tuwaeleze wananchi ukweli uliopo”,alisema RC Ndikilo.


Kuhusu suala la Meya Henry Matata kutoondolewa madarakani RC Ndikilo alisema kuwa hawezi kulizungumzia suala hilo kwa kuheshimu mamlaka ya mahakama na kuwataka chadema kuvuta subira hadi pale mahakama itakapotoa maamuzi yake.


KAULI YA MBUNGE KIWIA.

Akizungumza katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Kiwia alisema kuwa waliamua kuitisha maandamano hayo kutokana na kuelezwa na Waziri Hawa Ghasia kuwa tayari barua hizo zimeishatumwa mkoani Mwanza.


“Mheshimiwa Mkuu wa mkoa hawa madiwani waliosimamishwa ni wawakilishi wa wananchi,wamekaa nje kwa miezi saba sasa na uchaguzi wa Meya haukuwa halali ndio maana tuliamua kuitisha maandamano kwa ajili ya kuhakikisha madiwani hawa wanarejeshwa.


RPC MANGU.
Akizungumza kwa simu juu ya kutokea kwa vurugu zilizosababisha kupigwa kwa mabomu ya machozi,Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Ernest Mangu alisema kuwa polisi walifanikiwa kudhibiti vurugu hizo na hadi sasa hawezi kusema ni wananchi wangapi ambao walikamatwa kuhusu vurugu hizo.