Kwa wale watakao bahatika kulitembelea jiji la Washington, DC, hizi ni baadhi ya sehemu muhimu katika jiji hili kuweka katika orodha ya kuzitembelea.
Wednesday, May 19, 2010
Tuesday, May 18, 2010
Hivi kweli haya ni maendeleo au ni kuiga toka kwa wenzetu?
Kuna hatari ya kuupoteza utamaduni wetu kwa namna moja au nyingine kwani vitu vingi tulivyo na asili navyo vinatutoka taratibu bila ya sisi kujitambua! Vipi ugali na kisavu au makande? Taratibu kila kona ya miji yetu itakuwa imetawaliwa na migahawa ya kigeni... na hayo ndio maendeleo!!
Inavyotokea kwenye lugha zetu za kikabila ndivyo hata vyakula vyetu asilia vitakavyopotea. Katika miji yetu mingi vijana wengi walio kati ya umri wa miaka 18 mpaka 30, lugha za wazazi wao hazipandi tena. Tanzania tuna makabila 120 au zaidi sasa iweje asilimia kubwa ishindwe kuzungumza kwa kutumia lugha asilia?
Monday, May 17, 2010
Wednesday, May 12, 2010
Pichani: Mwenye Miwani Ras makunja kamanda wa Ngoma Africa band aka FFU katikati mwenye kofia nyeupe Afande Chris-B(Mshambuliaji wa solo) wa FFU na pembeni ni MR.Reginald Temu mwenyekiti wa chama cha urafiki kati ya wajerumani na watanzania akiwakaraibisha mjini Munich wageni wa hajabu !FFU wa Ngoma Africa ambao hawana uruma hata kiduchu washambuliapo jukwaani.bendi hiyo ya Ngoma Africa ilifanikiwa kuwatia kiwewe washabiki mjini munich usiku wa 8-05-katika shamra shamra za kusherekea kombe la soka la dunia Afrika Kusini 2010. Sherehe hizo ziliudhuriwa na wengi na wageni wa heshima walikuwa manaibu mabalozi wa tanzania na Afrika Kusini nchini Ujerumani, Naibu Balozi wa Tanzania uko Ujeruamani Mhe.Bw.Ali Siwa na Naibu Balozi wa Afrika Kusini nchini humo Mr.Martin Ngudze.
Wasikilze ngoma Africa band hapa http://www.myspace.com/thengomaafrica
Monday, May 10, 2010
Friday, May 7, 2010
Subscribe to:
Posts (Atom)









































