Thursday, October 30, 2008

Niko na waifu(wife) tunavinjari kwenye mnuso fulani. Life is good!!

Fikra za miaka minane aliyochemsha.



Hivi ndivyo ilivyokuwa jana wakati rais mtarajiwa Barak Obama na rais wa zamani Bill Clinton walipopanda jukwaani kwa mara ya kwanza wakiwa pamoja katika kuwahamasisha raia kupiga kura kwa wingi ili kumchagua bwana Obama, hapo ifikapo Jumanne Novemba 4, 2008.













Hawa ndugu zetu wa Jamuhuri ya Demokrasia ya Congo(D.R.C) bado wanaendelea kupigana wenyewe kwa wenyewe na ni raia wasio na hatia wa nchi hiyo ndiyo wanaondelea kuteseka. Hivi kweli Dunia imeshindwa kabisa kusaidia hili tatizo sugu la Afrika? Yanayoendelea Congo siyo tu kwamba yanawanyima haki zao raia wengi wa nchi hiyo, bali pia hali hiyo inazorotesha maendeleo ya Afrika nzima. Hili sio tatizo lao peke yao, bali ni la Afrika na Dunia nzima.




Tuesday, October 28, 2008


Kikumbi Mwanza Mpango "King KIKI", ni mmoja wa wakongwe wa musiki wa dansi Tanzania. Utunzi wa nyimbo na sauti yake viliwaburudisha wengi enzi hizo na hadi leo. Kwa walio wengi ni raha ndani ya roho kila tusikiapo nyimbo hizo. Mzee tunakushukuru sana kwa burudani.

Monday, October 27, 2008

Bi. Hennah wakati akiwa na miaka minne akipozi na mama yake. Tizama alivyopiga nne na tabasamu la mbali.







Ingawa ana miaka saba tuu, lakini binti huyu anaonyesha umaarufu mkubwa asimamapo mbele ya kamera. Amezaliwa Septemba 2nd, 2001 Jiji New York na kwa sasa yuko darasa la pili katika shule ya Ideal Montesori, Queens, NY.













Binti yangu Hennah Gabriella Ramadhani, akiwa katika mapozi ya nguvu katika kujitayarisha kupambana na kina Naomi na masupa modo wengine. Keep it up girl !!



Sunday, October 26, 2008


Siku zinakaribia na jamaa anaonekana anaelekea kwenye jumba jeupe.

Thursday, October 23, 2008

Naonekana nikiteta jambo fulani.... harusini Dar 2007.
Tunapokea vyeti toka kwa SVP of Executive Development Macy's East, baada ya kuhitimu mafunzo ya (Management Development Program).
Huyu jamaa vipi na ulimi? Unakumbuka ile picha aliyokosea njia ya kusuka jukwaani?

Siajabu haya ndio yakawa makazi mapya ya bwana Obama pindi ifikapo Januari 2009. Tulio wengi tunasubiri sana kuona mambo yatakuwaje siku ya uchaguzi na baada ya hapo. Kama Waswahili wasemavyo "kweli Mungu si Athumani".











Pamoja na ubaguzi mkali uliopo nchi hii, lakini wengi wa raia wa Marekani wameonyesha kumkubali bwana Obama. Tayari inadhihirisha wazi kwamba huyu bwana atakuwa rais
na kuingia kwenye vitabu vya historia kama mtu wa kwanza mweusi kuliongoza taifa hili kubwa lenye nguvu na utajiri mkubwa. Jambo hili linaleta matumaini makubwa ya kwamba kuna mambo mengi mazuri yanaweza kutokea Duniani. Thank you Dr. King, Mandela, Nnkruma, Nyerere na wengine wengi.


Tuesday, October 21, 2008



Baada ya kumalizika kwa mjadala wao wa mwisho (Octoba 15), mgombea Urais wa chama cha Republican bwana John McCain alionekana kupotea njia ya kushukia jukwaani na kuonekana kuchanganyikiwa kama picha hii inavyoonyesha.



Obama (katikati) akiwa na babu na bibi kwa upande wa mama yake wakati akiwa bado mwanafunzi.

Monday, October 20, 2008


Rusha roho.


Kisomo kabla ya ndoa kufungwa. Hapa ni mambo ya kanzu na barakashia na baadae inapita chai na maandazi ya nguvu.

Saturday, October 18, 2008


Mzee Kombo Ramadhani (wa pili kulia) akiwa na wadau kijijini Tanga.

Friday, October 17, 2008


Kufana kwa harusi ni kupongezana kwa kugonganisha gilasi za mvinyo

Wednesday, October 15, 2008



Sehemu ya MnaziMmoja, Dar inavyoonekana kwa mbali


Bwawa la Mtera ni moja ya chanzo kinachotoa umeme tutumiao Tanzania

Tuesday, October 14, 2008


Pamoja na tofauti zetu lakini "Sisi bado ni wamoja". Tuendelee kutafuta jinsi ya kuuimarisha na kuulinda UMOJA wetu.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Tuanamkumbuka Baba wa Taifa, mojawapo ikiwa ni jitihada zake kuliweka Taifa mbele katika kutetea haki za wengi kama alivyofanya kwenye matembezi ya kuunga mkono "Azimio la Arusha".

Saturday, October 11, 2008

Tuesday, October 7, 2008